aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Wednesday, February 26, 2014

CCM Matatani kwa Kuwapangisha watu wawili Kwenye fremu Moja.

CHAMA cha Mapinduzi (CCM)

CHAMA cha Mapinduzi (ccm), kimejiingiza matatani baada ya kuwapangisha wafanyabiashara wawili katika flemu moja la kufanyia biashara. Akizungumza jana jijini Dar es Salaammfanyabishara Charles Msigwa alisema aliingia mkataba na Mecy Mziray ambaye kwa sasa ni marehemu na aliendelea kumlipa kodi ndugu wa marehemu Vesta Haule. Alisema wakati akiendelea kufanya biashara katika banda hilo alishangazwa na viongozi wa CCM tawi la Vigaeni Kata ya Ndugumbi kumfuata wakitaka aingie mkataba upya na chama hicho.

Msigwa Afunguka

“Nimekuwa nikiendesha shughuli zangu za biashara kwa muda wa miaka minne ndipo nilipofuatwa na viongozi wa CCM na kunishauri nichukue mkataba nao ili chama kipate mapato,”alisema Msigwa.

CCM

Aliongeza kuwa viongozi hao walimuita kwenye ofisi ya tawi na kumuhakikishia hakutakuwa na tatizo lolote juu ya mkataba huo. “Viongozi hao waliniambia kuwa mabanda hayo hayarithishwi hata hivyo aliyeachiwa amekuwa msumbufu wa kodi mwenye banda alishafariki kwa hiyo banda huwa linarudi na kuwa mali ya chama,”alisema.
Msigwa alisema kuwa aliujaza mkataba huo na kuurudisha ofisini kwao alipotaka kuulipia akawa anazungushwa zungushwa. “Nilipeleka malalamiko yangu Kwa uongozi wa Wilaya ambapo uliwaandikia barua ya kwamaba wanitafutie banda jingine iwapo nikiwa tayari kutimisha masharti ya kuwa mpangaji wa chama hicho na nilikubali lakini uongozi huo haukufanya kama ulivyo agizwa,”alisema Msigwa.
Awali Chama cha mapinduzi (CCM) kiliingia mkataba wa kujenga banda hilo na Marehemu Mecy Mziray gharama zake na asingeweza kutoka mpaka gharama zake za ujezi zitakapo malizika.

No comments:

Post a Comment