aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Wednesday, February 26, 2014

Kibaka Anaswa Akiiba Kanisani Kijitonyama.


kibaka

Kibaka Anaswa

Kijana anayejulikana kwa jina moja la Emmanuel (30), amejikuta akipokea kipigo  kizito  baada ya kukamatwa akiiba katika Chuo cha Theofilo Kisanji ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kijitonyama, Dar.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni kanisani hapo, mchana kweupe ambapo Kibaka huyo ambaye amekuwa akifika mahali hapo mara kwa mara, alijikuta arobaini yake ikitimia na hivyo kutiwa mikononi mwa wanachuo ambao kabla ya kuhoji zaidi, walimshushia kipigo cha mbwa mwizi.
kibaka
“Huyu ndiye huwa anatuibia humu chuoni na kanisani, kila siku watu wanalalamika kuibiwa vitu vyao. Juzi tu, kuna watu waliibiwa simu, wengine fedha lakini hatukujua ni nani aliyekuwa akitufanyia hivyo, sasa huyu tutamkomesha,” alisema dada mmoja huku akiwa na furaha ya kukamatwa kwa jamaa huyo.
Wanachuo hao, wakionekana kupania kumfundisha adabu na kumwachisha Emmanuel udokozi, walikuwa wakimhoji maswali Kibaka huyo huku wakimwangushia kipigo mfululizo, hali iliyosababisha mwili kutoka damu nyingi iliyotapaa sakafuni kama buchani.
Kama kawaida, vijana  wetu hawakutaka kuishia kuangalia kipigo tu, waliwaita baadhi ya wanachuo walioibiwa mali zao na mashuhuda waliomuona kibaka huyo akiiba na kueleza mchezo mzima ulivyokuwa.
“Nilikuja hapa chuoni saa tisa (alasiri) nikaelekea mapokezi na baadaye darasani.
Nilipofika hapo, nikamuona mtu akisimama  ghafla, nikashtuka lakini sikutaka kuwa na wasiwasi sana, nilidhani ni mwanachuo wa hapa,” alisema msichana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Adolphina na kuendelea:
“Nikaondoka hapo na kupanda juu (ghorofani). Moyo wangu ukawa mzito, ghafla nikajikuta nikishuka ngazi na kurudi kule mapokezi. Nilipofika mapokezi, yule mtu niliyemuona pale hakuwepo, nilipoanza kumtafuta, nikaona akielekea getini kwa mwendo wa harakaharaka, hapo ndipo nilipoanza kupiga kelele za mwizi, naye akaanza kukimbia mpaka alipokamatwa,” alisema Adolphina.
Kibaka huyo alipopekuliwa begi alilokuwa nalo alikutwa na vyeti mbalimbali vya shule ya sekondari ya mkoani Mbeya, cheti cha kuzaliwa, cheti cha TRA na vyeti vingine vingi, vyote vikiwa si vyake.
Mbali na vyeti hivyo, pia alikuwa na kadi za mashine za ATM zikiwepo za CRDB, NMB na NBC, hali iliyoonesha kwamba huwa anazitumia kwa ajili ya kuchukulia ‘mkwanja’ kutoka katika akaunti za watu.
Alipopekuliwa zaidi mifukoni mwake alikutwa na simu aina ya Huawei yenye thamani ya shilingi 360,000 na Nokia Asha yenye thamani ya shilingi 150,000, ambazo zote ziliibwa ndani ya chuo hicho siku chache zilizopita.
 Askari wa Kituo cha Polisi Kijitonyama – Mabatini ndiyo walimuokoa jamaa huyo mikononi mwa wanachuo hao ambapo walifika eneo la tukio baada ya kujulishwa na mmoja wa watu walioshuhudia jamaa huyo akisulubiwa kwa hasira.

No comments:

Post a Comment