aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, February 20, 2014

Mama Wema Akesha Akiomba Diamond Afumaniwe..!!

MAMA wa Miss Tanzania 2006 aliye pia staa wa muvi za Bongo, Wema Sepetu, Mariam Sepetu amesema anamwomba Mungu bintiye huyo amfumanie mpenzi wake asiyemkubali, Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Amani  lina picha kamili.


Akizungumza na mapaparazi wetu juzikati jijini Dar es Salaam, mama Wema alisema:
“Najua kwa sasa sina tena mamlaka ya kuingilia mapenzi ya binti yangu kwani mambo hayo yamenichosha, yananiumiza na kichwa.

“Lakini naomba sana kwa Mungu itokee siku moja Wema amfumanie Diamond akiwa na mwanamke mwingine labda ndiyo itakuwa kikomo chao cha kuwa wapenzi kwani ndiyo ndoto ninayoiota kila siku.”

KWA NINI ANAOMBA DUA BAYA?
Mama Wema alikwenda mbele zaidi kwa kusema kwamba, amegundua binti yake huyo hana ubavu wa kuachana na Diamond hata kama atasikia ana mwanamke mwingine.

Mama Wema, Mariam Sepetu.

MAGAZETI PIA YAMESHINDWA
Mwanamke huyo anayemwogopa Mungu tu, alikwenda mbele zaidi kwa kusema kwamba, kuna wakati baadhi ya magazeti pendwa nchini yaliandika Diamond kuwa na demu mwingine lakini Wema hakukasirika wala kuachana na staa huyo wa muziki wa kizazi kipya.

MSIKIE MWENYEWE
“Kwa hiyo mchezo mzuri ni yeye (Wema) kumfumania huyo Diamond wake, maana magazeti tu  kuandika kwamba ana uhusiano na mwanamke mwingine mwanangu alivyofanywa mjinga wa kutupwa, hatamwacha.

“Mimi najua Wema anashindwa kukaa chonjo kwa sababu ndumba zimemtawala, amefunikwa labda baadaye atafunguka,” alisema mama Wema.

AIGUSA SAFARI YA DIAMOND NCHINI NIGERIA
Mama Wema akaanika jambo ambalo halijawahi kujulikana kabla.
Alisema: “Huyo Diamond ndo maana alikwenda Nigeria akashindwa kupiga muziki kwa sababu hakwenda na Wema, sasa ameona ampumbaze ili aweze  kwenda naye nchi za nje kwa masilahi yake binafsi, ataishia kumuahidi tu hana uwezo wa kumnunulia Wema kitu chochote chenye thamani kubwa, ni mpenda misifa tu.
“Si mnamjua huyo ni mtoto wa Tandale? Anajiita yeye m…(alitaja jina la kinyesi) na kweli yuko hivyo.

NDUGU WA DIAMOND WAMEJAZANA KWA WEMA
“Ndugu zake walivyo washamba wamejazana hovyo pale kwa Wema. Wajinga mno, maana mshamba siku zote ni mshamba,”     alisema mama huyo.

HATAKI KUSIKIA WEMA ANA MIMBA YA DIAMOND
Katika hali iliyoonesha kwamba kweli hampendi Diamond, Bi. Mariam alisema hataki kusikia binti ana ujauzito wa msanii huyo.

Alisema: “Mbegu (uzao) gani atakayoileta kwangu, huyo mjukuu si atakuwa balaa, siwezi kuharibiwa wajukuu. Mtoto asiyeeleweka siwezi kumshika.”

Wema.

ACHIMBA MKWARA
“Halafu nataka kuwaambia enyi watu wa magazeti, haya mambo ya kumwongelea huyo domo acheni mara moja, dunia itamnyoosha,” alisema.

AJIRUDI KWA MWANAYE
Mama Wema alisema hawezi kumlaumu sana binti yake  kwa vile akili si yake, yeye (Wema) ni mwanake na atabaki kuwa mwanamke, ila siku zote lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho.

DIAMOND SASA
Juzi, Amani lilimtafuta Diamond kwa njia ya simu na kumjulisha kuhusu ndoto za mama mkwe wake huyo ambapo aliishia kucheka.
“Teh! Teh! Teh! Thubutu.”

Diamond.

HAIJAWAHI KUTOKEA
Kumbukumbu za makabrasha ya Amani zinaonesha kwamba, katika historia ya wapenzi wa Wema, mzazi huyo hakuwahi kutokea kumkubali Diamond hata siku moja tu.
Amekuwa akimshukia mara kwa mara, madai yake siku zote ni kwamba, katika maono yake hajawahi kuona mapenzi ya kweli ya Diamond kwenda kwa Wema.
Japokuwa pia hajawahi kusema kama kuna mapenzi ya kweli ya Wema kwa Diamond.
Wema amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na marehemu Steven Kanumba, Jumbe Yusuf, Chalz Baba na Clement ‘kigogo wa ikulu’. Pia amewahi kudaiwa kutembea na TID na Mr Bluu.

No comments:

Post a Comment