aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Monday, February 17, 2014

MODEL WA TANZANIA HAMISA AZUNGUMZIA KUTOA PENZI KWA MWANAMUZI DIAMOND...HUYU HAPA

MREMBO anayedaiwa kuliingilia penzi la staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, aliyewahi kushiriki Shindano la Miss Tanzania, Amisa Mabeto amefunguka kuwa  mwanamuziki huyo ni shemeji yake tu, hakuna chochote kati yao.
Amisa Mabeto.
Akipiga stori na safu hii kuhusiana na madai hayo, Amisa alisema alistaajabu kwani hana mazoea na Diamond Kama ni kuonana waliwahi kuonana miaka ya nyuma, tena siyo kimapenzi.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
“Kamwe siwezi kutembea na Diamond na haitatokea kwani jamii nzima inajua yupo na Wema na mimi huyo mtu ni rafiki yangu mkubwa, hana chake hapa, siwezi kutembea naye kamwe, namheshimu kama shemeji yangu,” alisema Amisa.
Amisa aliwahi kuripotiwa kuwa na uhusiano na Diamond akiwa ni shosti mkubwa wa Wema.