aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Monday, February 10, 2014

MAPICHA:MAPENZI YA MKE WA MTU "CHUCHU HANS" NA RAY KIGOSI HADHARANI

MAMBO hadharani! Penzi ‘hoti’ la mastaa mahiri wa filamu za Kibongo, Chuchu Hans na Vincent Kigosi ‘Ray’ kwa sasa limekuwa kama la njiwa kwani mara nyingi kila sehemu wapo pamoja na hakuna kificho tena.
Ray na Chuchu wakijiachia.
Chanzo chetu makini kilieleza kuwa mastaa hao wamekuwa wakionekana pamoja mara nyingi na hivi sasa inadaiwa kuwa wanaishi pamoja huku wakiwa na mtoto wa Chuchu aitwaye Danzel.
Mpashaji wetu huyo alizidi kudai kuwa kutokana na mapenzi hayo kukolea siku hadi siku, juzikati baadhi ya ndugu wa mastaa hao walianza vikao vya chini kwa chini ili kuhakikisha mwaka huu wasanii hao wanafunga ndoa lakini haijajulikana kama watafungia kanisani au msikitini kwa kuwa wana dini tofauti.
“Yaani sasa hivi hakuna siri hata chembe, ni fulu kujiachia. Mara nyingi wapo pamoja kila sehemu yaani kama njiwa,” kilisema chanzo chetu.
 
Chanzo hicho kilizidi kudai kwamba mara nyingi Ray na Chuchu wanapenda kwenda kuogelea na kujiachia kama mke na mume kwenye hoteli moja maarufu (jina linahifadhiwa) iliyoko maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar huku wakijifotoa picha za kumbukumbu.
Baada ya kujazwa ‘info’ hizo na kumwagiwa picha za mastaa hao, gazeti hili lilimtafuta Chuchu kisha kumuuliza kuhusiana na penzi lake na Ray kuwa ‘shatashata’ ambapo alifunguka kuwa kama kuna mtu anawaona wakiwa pamoja ni kwa sababu hivi sasa eti wanaandaa ‘sinema’ yao wawili.
Alipotafutwa Ray ili kuulizwa kuhusiana na ishu hiyo, simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa kwa muda wa nusu saa

No comments:

Post a Comment