aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Monday, February 10, 2014

MAPENZI NOMA SANA : Jose Chameleone amuonesha mkewe 'Danniella' anavyompenda kwa kuchora tattoo ya jina lake shingoni


Wakati tunaelekea katika ile siku inayoaminika kuwa siku ya wapendanao ‘Valentine’s Day’, mkali wa Valuvalu Jose Mayanja Chameleone ameamua kumuonesha mkewe Daniella na dunia nzima jinsi anavyompenda, kwa kujichora tattoo yenye jina lake shingoni.
 
Chameleone ambaye yuko nchini Afrika Kusini kwa shughuli za kimuziki, alipost picha hizo kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, picha zinazoonesha tattoo hiyo hata mtu akimuona kwa mbali kidogo.
 
Mwimbaji huyo wa Valuvalu ambaye ana watoto watano aliozaa na mkewe Daniella hakuwasahau wanae pia, alijichora katika mkono wa kushoto tattoo yenye majina manne ya wanae wanne na anatarajia kuongeza moja yenye jina la mwanae wa kwanza, Ayla.
 
“2014 we stand tall for the ones we care for and those that love us back with their whole. For me, this is my expression..” Amesema Chameleone.