aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Wednesday, February 19, 2014

Baby Madaha atangaza kuachana na sanaa ya muziki na filamu kwa maelezo kuwa amechoshwa na maisha ya preshaIKIWA imepita miezi kadhaa tangu anaswe katika mtego  wa kujiuza,  staa wa Bongo, Baby Madaha ametangaza kuachana na sanaa ya muziki na filamu kwa maelezo kuwa amechoshwa na  maisha ya presha.

Akiongea  na  mwandishi wetu  juzikati jijini Dar es Salaam, Madaha alisema ishu ile imemsababishia matatizo makubwa ya kifamilia na hata kibiashara, hivyo kujutia mchezo mzima ulivyokuwa.
 
Alisema filamu anayoisambaza kwa sasa na kibao chake cha mwisho kukitoa cha Mr. Dj ndizo zitakazofunga pazia la mambo ya sanaa kwa upande wake.
 
“Nimeamua kuachana na sanaa kabisa, siwezi kuishi maisha ya presha yasiyo na uhuru. Nitarudi kwenye fani yangu niliyosomea (hakutaka kutaja), maana naishi maisha ambayo hayana amani kabisa,” alisema.