aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Tuesday, February 18, 2014

HATARI POSHO ZA SERIKALINI: WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA KUVUNA MILIONI 21...TSH 300,000/ KWA SIKU

HATIMAYE serikali imeweka hadharani kwamba kila mjumbe katika Bunge la Katiba ataweka kibindoni posho ya sh 300,000 kwa siku.


Kwa maana hiyo, kila mjumbe katika Bunge hilo atakuwa amelipwa sh milioni 21 kwa siku 70 za uhai wa Bunge hilo, na kama serikali itaongeza siku 20 zaidi kwa mujibu wa katiba na kufikia siku 90, kila mjumbe atavuna sh milioni 27.


Awali gazeti hili liliwahi kuripoti majadiliano ya ndani serikalini kabla ya jana kuthibitishwa rasmi ambapo kulikuwa na pendekezo la kutaka kila mjumbe alipwe sh 700,000 kwa siku.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Katibu wa Bunge Dk. Thomas Kashililah, alisema kuwa kila mjumbe katika Bunge hilo atalipwa sh 300,000 kwa siku.

Alisema malipo ya wajumbe hao ni pamoja na posho zote za vikao ikiwa imeunganishwa na posho za madereva.

Pia alieleza kuwa gharama zote ambazo zimetumika katika matengenezo ya ukumbi na sehemu nyingine ni sh bilioni 8.2 na fedha hizo ni bajeti ya kawaida ambayo ilipitishwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2013/14.

Mbali na hilo, Kashililah alisema kuwa kutokana na umuhimu wa kuwepo kwa Bunge Maalumu la Katiba, Bunge limehakikisha linafanya ukarabati ikiwa ni pamoja na kufunga mitambo mbalimbali ya usalama na kurekebisha mifumo ya kiutendaji.

Alisema matengenezo yaliyofanyika ni pamoja na kurekebisha paa la jengo la ukumbi wa Bunge ambalo awali lilikuwa likivuja wakati wa mvua.

Akitoa ufafanuzi zaidi katika ufungaji wa viti ndani ya ukumbi wa Bunge hilo, alisema  kuna viti 678 na kurekebisha vipaza sauti ambapo kazi hiyo pekee imegharimu dola za Kimarekani milioni moja.

Kuhusu maandalizi, alisema yamekamilika na wajumbe wameishaanza kufika bungeni kwa ajili ya usajili.

Alisema vikao vya Bunge vitaanza  rasmi Februari 18 majira ya saa nane mchana na wataanza kwa kumchagua mwenyekiti na makanu wake.

Alisema ratiba ya Bunge la Katiba itaanza na mkutano wa maelekezo kwa wajumbe Februari 18 asubuhi na Bunge lenyewe litaanza siku hiyo hiyo saa nane mchana.

Kwa mujibu wa katibu huyo, shughuli nyingine zitakazofanyika ni pamoja na mwenyekiti wa muda kusimamia uandaaji  na upitishwaji wa kanuni.
Alisema mwenyekiti wa muda atasimamia uchaguzi wa mwenyekiti na baada ya kupatikana mwenyekiti na makamu wake, ndipo atakapopatikana katibu ambao wataapishwa na Rais Jakaya Kikwete.
Uhai wa Bunge hilo utakoma Aprili 30 au kwa ridhaa ya rais.
-Tanzania Daima

No comments:

Post a Comment