aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, February 7, 2014

JACK CHUZ AWAPA MAKAVU WATU WANAOMLAUMU KWA KUTOZAA BAADA YA KUKAA KWENYE NDOA MWAKA MMOJA

Msanii wa filamu za Kibongo, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ amewapa makavu laivu baadhi ya watu wanaoshangaa na kuhoji inakuwaje anatimiza mwaka mmoja ndani ya ndoa bila kuzaa.
  
Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ akiwa na mumewe siku ya ndoa yao.
Akizungumzia maneno ambayo amekuwa akiyasikia kutoka hata kwa watu wake wa karibu wakiwemo wasanii wenzake, Jack alisema anawashangaa kwa kuwa wanashindwa kujua kwamba kuolewa ni sheria lakini kuzaa ni majaliwa.

“Ni kweli ndoa yangu keshokutwa tu inatimiza mwaka mmoja lakini nawashangaa wanaohoji kutokuzaa kwangu, wao wako nje ya ndoa hawajui mambo yanaendaje, wakiingia watajua kuwa kuzaa ni majaliwa ya Mungu,” alisema Jack.