
MSANII ambaye anang’ara kupitia Mchezo wa Green Message unaorushwa na Kituo cha Televisheni cha TBC, Daniel Mmasi ‘Face Brown’ (pichani) amelikimbia kundi la Tuesday Kihangala ‘Mr Chuz’, Tuesday Intertainment kwa sababu ya ukata.
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Face alisema alipokuwa akilitumikia kundi hilo, alikuwa hapati kitu chochote hivyo akatimka na wenzake kwenda kuanzisha kundi jipya la Green Massage.
“Niseme tu ukweli, hakuna kitu kilichonitoa kwa Mr Chuz zaidi ya njaa. Kama ningeendelea kuwa pale sijui ingekuwaje mpaka sasa, maisha yalikuwa magumu kuliko maelezo,” alisema Face Brown.CHANZO: GPL
No comments:
Post a Comment