aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Tuesday, July 30, 2013

KWA NINI MAOFISA USALAMA WANAUAWA KIRAHISI?!!

WANANCHI wengi walioshuhudia Afisa Usalama wa Taifa  akiuawa Tegeta Kibaoni jijini Dar Ijumaa iliyopita, waliuliza kwa nini maofisa  wa idara hiyo siku hizi wamekuwa wakiuawa kirahisi?

mwili wa Ramadhani Mrutu ukiwa umefunikwa

Hakukuwa mwenye jibu sahihi na badala yake wakawa wanaikodolea macho maiti ya afisa huyo aliyetambulika kwa majina ya  Ramadhani Mrutu ambaye alikuwa amepigwa risasi mchana kweupe na watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi maeneo hayo ya Tegeta kibaoni.
Wananchi hao walikuwa wakirejea kifo kingine chenye utata cha Afisa Usalama wa Taifa, Peter Tyenyi ambaye maiti yake ilikutwa kisimani karibu na ofisi zao zilizopo Kijitonyama jijini Dar Mei 27, mwaka huu. Hadi leo hakuna chombo chochote cha dola kilichotoa taarifa kuelezea kilichomuua afisa huyo.
Waandishi wetu waliokwenda Tegeta Kibaoni mara tu baada ya kupata habari za kuuawa kwa afisa Mrutu, waliambiwa na mashuhuda kuwa alipofika kwenye gereji moja ambayo huwa anaitumia kutengeneza gari lake alivamiwa na mtu mmoja aliyekuwa na bastola.
“Yule jambazi alimnyang’anya mkoba aliokuwanao kisha kumpiga risasi tatu, wengi tulishituka sana tuliposikia milio ya bunduki,” alisema shuhuda aliyeomba jina lake lisiandikwe gazetini.
 Chanzo chetu cha habari kilisema kuwa ofisa huyo alikuwa ametokea benki kuchukua fedha ambazo kiasi chake hakikufahamika mara moja na alipotoka hapo alienda moja kwa moja katika gereji ambayo mauaji yalifanyika.
 “Inaonekana mtu aliyemuua akiwa na dereva wa pikikipi walitoka naye mbali hadi kufika naye pale gereji na kufanya unyang’anyi na mauji hayo,” kilisema chanzo hicho.
Kikaongeza Mrutu alipigwa risasi saa 6.15 mchana, risasi ya kwanza ilimpata mguuni, ya pili kiunoni, ya tatu kifuani hali iliyosababisha kifo chake palepale.
Kiliendelea kutiririkia kuwa, baada ya unyama huo majambazi hayo yaliondoka na begi dogo alilokuwa nalo na kutokomea kusikojulikana.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP  Camilius Wambura aliliambia gazeti hili kuwa upelelezi juu ya tukio hilo unaendelea.
“Tunafanya upelelezi ili tuweze kuwatia mbaroni wahusika,” alisema Kamanda Wambura alipopigiwa simu na gazeti hili.

No comments:

Post a Comment