aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Tuesday, July 30, 2013

WALIOMMWAGIA TINDIKALI MAMA NA MTOTO WAKE WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 44 JELA...!!


Kundi moja ambalo lilikuwa likicheka huku wakimlowesha mwanamke mmoja kwa tindikali wakati mama huyo akiwasindikiza nyumbani watoto wake mapacha wenye miaka sita kutoka shuleni, wamehukumiwa kifungo cha jumla ya miaka 44 jela. 
Washambulizi hao walisikika wakicheka huku kimiminika hatari kikifukiziwa kwa mama huyo aliyekuwa akipiga kelele za uchungu mbele ya watoto wake wawili wa kiume nje ya Shule ya Msingi ya Upton Cross mjini Upton Park, mashariki mwa London.
 
Akizungumza baada ya shambulio hilo mwanamke huyo, ambaye aliungua vibaya usoni na mwilini mwake, alisema: "Nilimwona mwanaume akinikabili ambaye alikuwa amebeba kitu fulani ndani ya chupa.
 
"Alinirushia na baada ya sekunde chache ikaanza kuniunguza. Nilikuwa nikilia: "Tafadhali nisaidieni! Tafadhali nisaidieni!"
 
Inadhaniwa Yannick Ntesa, mwenye miaka 25, alifukiza tindikali hiyo na kutoweka ndani ya gari lake aina ya BMW lenye rangi nyekundu akiwa na Abdul Motin, miaka 28, na Ahad Miah mwenye miaka 31.
 
Mama huyo mwenye miaka 44, kutoka Plaistow, alikimbilia kwenye nyumba moja ya jirani ambako maji yalimwagiwa kwenye nguo zake zilizokuwa zikiungua.
 
Baadhi ya tindikali iliunguza mkoba wa mtoto wake wakatimama mwingine pia alipata majeraha madogo katika shambulio hilo lililotokea Machi 24, 2011.
 
Muathirika huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Royal London na baadaye akahamishiwa kwenye kitengo cha mtaalamu mmoja wa majeraha ya moto huko Chelmsford, Essex.
 
Ameathirika asilimia 16 ya kuunguzwa na kemikali hiyo na bado anapatiwa matibabu.
 
Kufuatia kesi iliyochukua wiki sita kwenye Mahakama ya Blackfriars korti imewatia hatiani Ntesa, Motin na Miah kwa shambulio la kudhuru mwili na kumrushia mwingine kimiminika hatari kwa kudhamiria.
 
Motin, kutoka Stepney, mashariki mwa London, alihukumiwa kifungo cha miaka 16 jela.
 
Ntesa, kutoka Paddington, na Miah, ambaye hana makazi maalumu, wote walihukumiwa kifungo cha miaka 14 jela.
 
Hakuna sababu yoyote ya shambulio hilo iliyotolewa lakini Inspekta Mpelelezi John Reynolds, wa Ofisi ya Upelelezi ya Newham, alisema: "Hakika hili ni shambulio ya kushitusha kwa mama ambaye alikuwa na watoto wake wadogo mno wawili sambamba nao wakati huo.
 
Naomi Oni, mwenye miaka 21, ambaye alikuwa akifanya kazi Westfield Shopping Centre huko Stratford, alikaa mwezi mzima hospitalini baada ya shambulio la tindikali huko Dagenham, Essex, saa za mapema Desemba 30, mwaka jana.
 
Mnamo Aprili, mwanamke mmoja aliyetambuliwa kama Tara, alimwagiwa tindikali usoni baada ya kumfungulia mlango mgeni nyumbani kwake huko Romford
.


No comments:

Post a Comment