aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Wednesday, July 31, 2013

MBONI AANGUA KILIO MBELE YA MZEE RUKSA

 HOSTI wa Kipindi cha ‘The Mboni Show‘ kinachorushwa kupitia Kituo cha Runinga cha EATV,  Mboni Masimba Jumapili iliyopita aliangua kilio mbele ya Rais Mstaafu wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi walipokuwa kwenye hafla ya kufuturisha kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Mtangazaji huyo alimwaga machozi wakati akiwakaribisha wageni waalikwa pamoja na kutoa shukrani zake kwa wote waliomsaidia kufanikisha shughuli hiyo.
Baada ya kutoa shukrani alionekana kuwa mwenye
furaha kwa kumtambulisha baba yake mzazi, mzee Masimba ambaye hajulikani kwa watu kama ilivyo kwa mama yake.Aidha, mtangazaji huyo alimwita mama yake, bila ya kutarajiwa akaanza kumuomba msamaha mzazi wake huyo kwa kumsumbua na kumuahidi kwamba amejirekebisha.
“Nakuomba msamaha mama yangu, Mboni si yule tena nimebadilika, nisamehe sana,“ alisema Mboni kisha akaangua kilio kujutia makosa yake.
Baada ya tukio hilo, Mboni alisikika akiomba dua kwa Mwenyezi Mungu ili ampe mume mwema. Mtangazaji huyo alirudia mara kwa mara kipengele hicho cha kuomba mume kiasi cha baadhi ya wageni waalikwa kusema kwamba ni kweli anahitaji mume kwani umri wake unahitaji kuwa na familia.Mbali na matukio hayo, Mboni alitambulisha vituo viwili vya watoto yatima ambavyo anavihudumia kupitia kampuni yake ya The Mboni. Mbali na Mwinyi wageni wengine walikuwa ni Shehe wa Mko wa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, Asha Rose Migiro pamoja na Khadija Mwanamboka.
Wengine ni Shay-rose Bhanji na baadhi ya wanamuziki wa The Kilimanjaro ‘Wana Njenje’ Steve Nyerere na watu wengine maarufu.
NA GLOBAL PUBLISHERS 

No comments:

Post a Comment