aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Sunday, July 28, 2013

Mastraika hawa sita watauana Jangwani

 KAMA kuna nafasi ngumu kwenye kikosi cha mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga msimu ujao, basi ni nafasi ya ushambuliaji.
 Yanga mpaka sasa  ina washambuliaji sita na uongozi wa klabu hiyo umepanga kuongeza mmoja wa kigeni.
Washambuliaji waliopo ni Jerryson Tegete, Didier Kavumbagu, Shaban Kondo, Said Bahanuzi, Mrisho Ngassa na Hussein Javu. Kama haitoshi  klabu hiyo bado inaendelea na mazungumzo na Hamis Kiiza huku pia  straika wa Uganda anayedai dau kubwa, Moses Oloya, naye akitarajiwa kutua klabuni hapo. Lakini Oloya ana uwezekano wa  kwenda Simba pia. 
Yanga itaachana na mshambuliaji raia wa Nigeria, Brendan Ogbu, kwa vilen amekuwa majeruhi hivyo kushindwa kulishawishi benchi la ufundi.
 Kocha wa Yanga, Ernest Brandts, aliiambia Mwanaspoti jana Ijumaa kuwa ushindani baina ya mastraika ni mzuri kwani utachochea wachezaji wake kujituma zaidi na kugombea namba.
“Wapo wengi lakini ni faida pia kwani watajituma kwa kuhofiana wao kwa wao, kila mmoja atataka kucheza, hivyo itasaidia timu kuwa na washambuliaji wenye uchu wa mabao kwani hakuna hata mmoja ambaye atataka kuanzia benchi,”alisema Brandts.
Aliongeza: “Kila mara nimekuwa  nikilalamikia washambuliaji, lakini sasa naona mwanga mzuri mbele kwani wako wengi na naamini watafanya kazi.”
Jerry Tegete
Amekuwa na misimu miwili mibaya na ametupia lawama matatizo ya goti kuwa ndiyo yalishusha kiwango chake.
Sasa amepanga kuibuka upya msimu ujao huku akikiri kuwa kazi itakuwepo kwenye nafasi hiyo, lakini hahofii  kwani anasema kazi yake itakuwa kupiga mabao tu.
Didier Kavumbagu.
 Alianza vizuri mzunguko wa kwanza msimu uliopita alipopachika mabao manane, lakini mzungukko wa pili alifunga mabao mawili tu na kumaliza katika nafasi ya pili kwa ufungaji akiwa amefunga mabao 10.
Amerudi kwenye fomu sasa kwani amekuwa akifunga mazoezini na kwenye mechi za kirafiki.
Mrisho Ngassa
Wimbi la majeruhi ndiyo kitu pekee kinachoweza kumnyima namba kwenye kikosi cha kwanza, lakini vinginevyo ana namba ya uhakika.
Ameonyesha kiwango cha kuvutia kuanzia mazoezini na ni chaguo la kwanza la benchi la ufundi.
Shaban Kondo
Alisajiliwa hivi karibuni kutoka Msumbiji alikokuwa akicheza soka la kulipwa. Ana umbo kubwa na urefu mzuri unaostahili kwa mshambuliaji, amefunga mabao mazoezini na kwenye mechi za kirafiki. Kocha ameonekana kumkubali na kumpa mbinu zaidi kila mara.
Said Bahanuzi
Anajulikana kwa jina la Straika wa Kagame baada ya kutisha sana kwenye michuano hiyo iliyofanyika mwaka jana na kuibuka mfungaji bora.
Lakini  alipotea baadaye. Alifunga bao moja tu kwenye  Ligi Kuu msimu uliopita tena kwa penalti katika mechi ya watani wa jadi Yanga na Simba. Kwenye mazoezi ya hivikaribuni ameonyesha kiwango kizuri.
Hussein Javu
Ni mshambuliaji mpya kutoka Mtibwa Sugar, amepata nafasi ya kusajiliwa na klabu hiyo baada ya kuonyesha uwezo mkubwa katika mechi mbili dhidi ya Yanga na Simba ambazo zote alitupia magoli nyavuni kwenye ligi iliyopita.
Makipa wajazana

Makipa wa Ligi Kuu Bara wamiminika na kurundikana katika kikosi cha Yanga kwa ajili ya mazoezi chini ya kocha Mkenya Razack Siwa.
 Walinda mlando hao ni pamoja na Msafiri Davo aliyekuwa Kagera Sugar, Nelson Kimath aliyeidakia Yanga miaka ya nyuma wameungana na Deogratius Munishi ‘Dida’,  Yusuph Abdul na Juma Kazembe.
Siwa aliliambia Mwanaspoti akisema: “Wapo wengi ambao wanahitaji kuja kufanya mazoezi hapa tunawaangalia, mambo ya usajili wao sijui lolote.”
Siwa ameongeza kuwa, hata kipa wa zamani wa klabu hiyo na Taifa Stars, Ivo Mapunda ambaye kwa sasa anaichezea Gor Mahia atajifua hapo.
Naye, Kimath amesema: “Nimeamua kuja kujifua hapa kwa sababu Siwa ni kocha mzuri nimekuwa namjua kwa kipindi kirefu alinifundisha miaka ya nyuma nilipokuwa nacheza hapa.”
Kutokana na hali hiyo, kocha Brandts anaamini kuwa timu yake inazidi kuimarika na haoni kama atakuwa na tatizo lolote la kutetea ubingwa wa Bara msimu mpya na hata kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa.
“Mwenendo wa timu katika maandalizi yetu uantia moyo, tunaendelea na kazi ya kuiimarisha timu ili kazi ikianza basi tuwe na msimu bora, tunataka msimu bora pengine kuliko yote iliyotangulia,” alisema kocha huyo akiwa na matumaini makubwa. 

No comments:

Post a Comment