Napoli wameonyesha kwamba wana nia ya dhati ya kupambana kwenye michuano mikubwa ya barani ulaya kwa kufanya usajili mkubwa wa mshambuliaji wa kiargentina kutoka kwa miamba ya soka ya Hispania.
Hii sentensi inaweza ikawa sawa na iliyoandikwa mwaka 1984 wakati aliposajiliwa Diego Maradona kutoka Barcelona - 2013 wamemsajili muargentina mwingine Gonzalo Higuain kutoka. Hii inaonyesha klabu hii imejidhatiti kutoa ushindani mkubwa kwenye mashindano makubwa barani ulaya.
Ndio, Edinson Cavani, mfungaji wa mabao 29 katika mechi 34 za Serie A msimu uliopita, ameondoka kwenye klabu hiyo na kujiunga na PSG kwa ada ya uhamisho wa£55million, fedha iliyopatikana kupitia mauzo ya Cavani imempa kocha wa klabu hiyo Rafael Benitez, kukiboresha kikosi chake ili kiweze kushindani kugombea kombe la Serie A na kutoa ushindani mkubwa kwenye Champions League.
Ni mara mbili tu kwenye historia ya klabu hiyo imeweza kushinda ubingwa wa Serie A – msimu 1986/87 na 1989/90 – mara zote mbili walikuwa wakiongozwa na vipaji vilivyokuwa vikiongozwa na gwiji Maradona.
Miaka mitatu iliyopita klabu hii iliweza kuanza kujipanga upya na kurudi kwa kasi kwenye ushindani wa soka la kimataifa, waliweza kucheza kucheza kwenye mashindano makubwa kwa ngazi ya vilabu barani ulaya - Champions League kuanzia msimu wa 2011/12 - msimu ambao walikuwa na safu nzuri ya ushambuliaji iliyokuwa ikiongozwa na Cavani, Ezequiel Lavezzi, na Marek Hamsik.
Waliwatoa Manchester City nje ya mashindano mwaka huo japo walifungwa na Chelsea timu ambayo ilienda kushinda ubingwa wa ulaya msimu huo.
Msimu uliopita, pamoja na kuondokewa na Lavezzi aliyeenda PSG, waliweza kumaliza nafasi ya pili kwenye Serie A nyuma ya mabingwa Juventus.
Je Higuain ataweza kufuata nyayo za aliowarithi na kusaidia kupanda nafasi moja juu kwa maana ya kubeba ubingwa? Kwa hakika hana kipaji binafsi kama alichokuwanacho Maradona lakini rekodi ya mabao yake inambeba. Alifunga mabao 107 katika michezo 190 akiwa na Real baada ya kuhamia akitokea River Plate mwaka 2006.
Rekodi hii nzuri ndio iliyomvutia hata Arsene Wenger kutoa ofa ya kutaka kumvuta muargentina huyo Emirates. Maslahi binafsi inaaminika yalishafikiwa lakini Real wakaongeza bei na mwishowe Napoli, wakiongozwa na mwenyekiti wake Aurelio De Laurentiis, wakamnyakua mshambuliaji huyo.
Amewagharimu £32million lakini ada hiyo ni haki yake ukiangalia utajiri wa uzoefu anaokuja nao akiwa bado kijana mdogo mwenye miaka 25.
Nafasi yake ndani ya Real Madrid ilikuwa finyu, hvyo alihitaji kutafuta sehemu ambayo angepata nafasi kubwa ya kucheza. Pia nafasi ya kufanya kazi chini ya Benitez, mshindi wa kombe la mabingwa wa ulaya na Europa League - ilichangia mshambuliaji huyo kuvutiwa na Napoli.
Pepe Reina, mtu ambaye amekuwa golikipa namba moja wa Liverpool kwa muda mrefu, mshindi wa kombe la ulaya na dunia, amejiunga na klabu hiyo kwa mkopo. Wachezaji wenzie wa zamani wa Real Raul Albiol, ambaye hucheza nafasi ya beki wa kati na Jose Maria Callejon, winga wa kulia nao wameungana na Higuain.
Dries Mertens, winga wa kushoto wa Ubelgiji - nae yupo kwenye kikosi hiki cha mapinduzi cha Rafael Benitez. Hamsik bado yupo ndani ya kikosi.
Bara la ulaya inabidi wakae tayari, mwezi mwingine wa bluu unaibuka kwa kasi nchini Italia.
Tuesday, July 30, 2013
MWEZI MWINGINE WA BLUU UNAIBUKA - MIAKA 29 BAADA YA MARADONA - SASA NI ZAMU YA HIGUAIN KUFUATA NYAYO ZA GWIJI WAKE NDANI YA NAPOLI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment