aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Sunday, July 28, 2013

Epiq BSS yamaliza usaili wake, kuanza mchujo wiki hii.




Majaji wa Epiq Bongo Star Search Master J, Salama Jabir na Chief Judge Madam Ritha Paulsen wakifurahi jambo wakati wa usaili wa vijana wa Dar es Salaam uliofanyika uwanja wa Taifa.



Wasichana hawa ni mapacha ambao walijitokeza kwenye usaili wa shindano la Epiq Bongo Star Search (EBSS) uliofanyika kwenye uwanja wa taifa Dar es salaam, walilazimika kuimba pamoja na ni tukio la kwanza kwa washiriki wawili kuimba pamoja kwenye usaili wa mwaka huu.



Wasichana hawa mapacha waliojitokeza kwenye ushiriki wa shindano la EBSS 2013 mkoani Dar es salaam wakisikiliza jambo kutoka kwa Jaji Mkuu wa EBSS Ritha Paulsen.



Mwanafunzi wa kidato cha nne katika sekondari ya Yusuph Makamba, Dar es salaam akifurahi baada ya kupita awamu ya kwanza ya shindano la EBBS 2013.



Umati wa vijana wakisubiri kufanyiwa usaili.



Umati wa vijana uliojitokeza kwenye usaili wa EBSS 2013 kwenye uwanja wa taifa.



Mtangazaji wa Clouds Radio Millard Ayo ambaye naye alishiriki katika kutoa maamuzi kwenye usaili huo akishow love na Majaji w EBSS mara baada ya kumaliza zoezi la usaili jijini Dar kwenye Uwanja wa Taifa.

Shindano la kuimba la Epiq BSS limemaliza usaili wake ambao kwa mwaka huu umefanyika katika mikoa sita ya Arusha, Mbeya, Mwanza, Zanzibar, Dodoma na kumalizia Dar es Salaam.

Usaili wa Dar es Salaam uliofanyika mwishoni mwa wiki hii ndio umehitimisha zoezi la kusaka vipaji, huku mwishoni mwa wiki hii washiriki wakijiandaa kuingia kambini kwa ajili ya mchujo wa kwanza.

Wiki hii washiirki waliopatikana mikoani wataungana na washiriki wa hapa Dar es salaam katika mchujo wa awali wa kupata washiriki watakaoingia katika kambi rasmi ya EBSS 2013.

Kwa mkoa wa Dar es salaam washiriki waliopatikana ni 20 huku mikoa mingine ya Arusha, Mwanza, Dodoma, Mbeya na Zanzibar washiriki waliopatikana ni sita kila mkoa hivyo kufanya jumla wa washiriki watakaoingia katika mchujo wa awali kuwa 50.

Shindano hilo ambalo mwaka huu lilikuwa na utaratibu mpya wa kutumia majaji wenyeji kutoka katika kila mkoa, ambapo kwa upande wa Mbeya kulikuwa na majaji ambao ni watangazaji wa radio huku usaili wa Dar es Salaam ukichagizwa na mchezaji wa mchezo wa mpira wa kikapu wa ligi ya Marekani (NBA) Hashim Thabeet aliyekuwa kama jaji mwalikwa.

Akizungumza na baadhi ya wahiriki waliojitokeza Hashim aliwataka vijana kutokata tamaa katika kutafuta mafanikio kupitia muziki.

Alisema kuwa anaamini Tanzania kuna vipaji vingi vya muziki ambavyo vinatakiwa kuendelezwa kufikia viwnago vya kimataifa, lakini ili kufanikisha hilo inatakiwa vijana wenyewe kujiamini na kuongeza nia ya kweli katika kutafuta kung’arisha nyota zao.

Aliwataka kutambua kuwa nidhamu na kujituma ndio siri kubwa ya mafanikio katika sanaa na kazi yoyote ile na hivyo aliwasihi kujitambua na kutafuta mfanikio hayo.

Akizungumzia shindano hilo kwa mwaka huu, jaji mkuu wa shindano hilo, Ritha Paulsen alisema mchuano utakuwa mkali hasa kutokana na kuchagua washiriki wakali kutoka kila mkoa.

‘Mwaka huu ushindani utakua mkali kuliko mwaka jana, lakini pia kutakuwa na burudani zaidi kutoka kwa washiriki kama ambavyo imezoeleka’ alisema Ritha.

Naye Afisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan alisema Zantel imezidi kuboresha shindano hilo, huku akiwataka watanzania watarajie makubwa zaidi mwaka huu katika kuzalisha vipaji na pia kupata burudani kubwa.

‘Tutatoa zawadi kadha wa kadha shindano litakapoanza, lakini pia wale ambao bado wanataka kushriki wanaweza kutumia njia ya simu kufanya usaili wao’ alisisitiza Khan.

Washiriki wanaotaka kufanya usaili kwa njia ya simu wanapaswa kupiga namba 0901551000 au watume ujumbe mfupi kwenda 15530 kupata maelezo ya namna ya kujiunga.

No comments:

Post a Comment