aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Monday, July 29, 2013

KOCHA WA SIMBA MFARANSA PATRICK LEIWIG KURUDI BONGO KUFUNDISHA SOKA










































Aliyekuwa kocha wa Simba mfaransa Patrick Leiwig anatarajia kutua nchini kurudi 
kufundisha soka katika klabu ya African Lyon.

Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika kutoka chanzo cha habari kilicho karibu na African Lyon ni kwamba klabu hiyo kwa sasa ipo kwenye mazungumzo mazito na kocha huyo aliyebobea katika kukuza vipaji vya wachezaji makinda.

"African Lyon pamoja na kushuka daraja lakini ni timu ambayo inafanya mambo yake kwa kuangalia mbele zaidi. Sasa wameamua kuwekeza zaidi kwenye timu zao za vijana na ndio maana wanaamua kumchukua kocha ambaye ana uzoefu mkubwa wa kukuza vipaji vya wachezaji makinda. 

"Mpaka sasa mazungumzo yanaendelea vizuri na siku chache zijazo tutegemee kumuona Leiwig akitua Bongo kuja kuiongoza African Lyon," kilikaririwa chanzo hicho cha habari.

No comments:

Post a Comment