aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, July 27, 2013

DIWANI AFUMANIWA HUKO IRINGA ACHEZEA KIPIGO


Katika hali isiyo kuwa ya kawaida diwani mmoja wa chama cha siasa jina lake na chama chake limewekwa kapuni kwa sasa amefumaniwa akivunja amri ya sita na mke wa mtu usiku wa leo na kuchezea kichapo .


Diwani huyo mpenda ngono anadaiwa kufumaniwa akiwa katika nyumba ya mpiga kura wake huyo katika kata moja ya wilaya ya Iringa Vijijini na ni diwani anayetokea katika wilaya ya Iringa mkoa wa Iringa na ni diwani mtanashati kweli kweli.


Mashuhuda wa tukio hilo wameudokeza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kuwa kutokana na fumanizi hilo la mwaka wapiga kura wake wanaoishi jirani na nyumba hiyo ambayo mheshimiwa alifunaniwa waliizunguka nyumba hiyo na kuanza kumshikisha adabu mheshimiwa huyo.


Baada ya mheshimiwa huyo kuchezea kipigo kutoka kwa njema lenye mke huyo pamoja na wananchi alilazimika kutoka mbio na kukimbilia porini kabla ya kwenda kupatiwa matibabu katika moja kati ya zahanati mbili zilizopo katika eneo hilo ikiwemo ya Misheni na ile ya Kijiji .

Pichani ni moja kati ya picha ya fumanizi ambayo inafanana na fumanizi hili la diwani japo hainamahusiano na tukio hili

No comments:

Post a Comment