aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Sunday, January 5, 2014

Hatimaye Aliyewahi kujaribu kujinyonga mara mbili afanikiwa kujiua...!!

BIBI kizee aliyefahamika kwa jina la Emmy Mjenzi (106) mkazi wa Mtaa wa Mhuti Kijiji cha Chigongwe wilayani Bahi, mkoani hapa amekufa kwa kujinyonga chumbani kwake kwa kutumia kamba ya mbuyu iliyosokotwa kwa kile kilichodaiwa kuchoka kuishi kwa muda mrefu.
Tukio hilo limethibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Suzan Kaganda alisema tukio hilo lilitokea Januari mosi mwaka huu majira ya saa 12 jioni katika kitongoji cha Mhuti.
Alisema Emmy aliwahi kujaribu kujinyonga mara mbili Mei na Novemba mwaka jana, lakini aliokolewa. Kaimu Kamanda alisema sababu ya kujinyonga ni kuchoka kuishi kwa muda mrefu na uchunguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea.
Katika tukio lingine, Kamanda Kaganda alisema lilitokea Desemba 31, mwaka jana saa mbili usiku katika Kijiji cha Ndalibo, Kata ya Mtanana Wilaya ya Kongwa mkoani hapa ambapo Kamota Chimasi (50) ambaye ni Mkulima na mfugaji aliuawa kwa kupigwa risasi mgongoni kwa bunduki aina ya Gobore na watu wasiofahamika wakati akiwa nje ya zizi akihesabu ng’ombe wake.
Alisema katika tukio hilo hakuna kilichoibiwa na chanzo cha mauaji hayo bado hakijafahamika. Pia alisema watu watatu wanashikiliwa na Polisi kwa mahojiano pamoja bunduki aina ya gobore na upelelezi unaendelea kubaini chanzo na sababu ya tukio hilo.
Kaimu Kamanda alisema hakuna mtu aliyekamatwa na upelelezi wa tukio unaendelea. Aidha alisema tukio lingine , alisema mtoto wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Mwenge, Manispaa ya Dodoma, Irene Simphorian (7) amekutwa akiwa amekufa porini baada ya kutoweka nyumbani kwao.
Alisema tukio hilo lilitokea Desemba 31, mwaka jana katika mtaa wa Mbabala “A” Kijiji cha Mbabala ambapo mtoto huyo alipotea katika mazingira ya kutatanisha nyumbani kwao baada ya kuachwa peke yake na wazazi na alipatikana Januari mosi mwaka huu akiwa amefariki dunia eneo la pori la jirani umbali mita 300 kutoka nyumbani kwao pia ni jirani na Kanisa la Anglikana.
Alisema hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo na uchunguzi wa mwili wa marehemu unafanyika na upelelezi zaidi juu ya tukio hilo unaendelea.

Credit: Habari Leo 

No comments:

Post a Comment