aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, January 23, 2014

Sangoma Matatani kwa Wizi wa watoto wadogo huko Jijini Mwanza..!!

MGANGA wa kienyeji ‘Sangoma’aitwaye Ramadhani Issa (20) amedaiwa kuwatorosha watoto wawili, Salim Swalehe(13) na LaurentOscar (13) wanaosoma katika Shule yaMsingi ya Pamba jijini hapa.
Sangoma Ramadhani Issa (20) akiwa chini ya ulinzi baada ya kunaswa.
Tukio hilo limetokea Januari 20, mwaka huu katika kitongoji cha Ujaluoni, Igogo jijini hapa baada ya watoto hao kutoonekana kwa mwezi mzima tangu Desemba 27, mwaka jana.
Inadaiwa kwamba watoto hao walirudi makwao kwa njia za ajabu na kusema walikuwa wamewekwa ndani kama misukule  nyumbani kwa mganga huyo.
Watoto waliokuwa wametekwa na sangoma Ramadhani Issa.
Wazazi wa watoto hao wanaoishi Mabatini, waliomba msaada kwa Kitengo cha Oparesheni cha Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers kumnasa mganga huyo.
OFM wakiwa na mtandao wa kijamii wa Farijika, waliambiwa na watoto hao kwamba walichukuliwa na mganga huyo Desemba 27, mwaka jana wakiwa katika matembezi ya sikukuu.
“Mganga alitugusa na shanga vichwani na kutufanya tupoteze kumbukumbu na kumfuata kila alipokuwa akienda,” alisema Laurent.
Hapa ni ndani ya getho la Sangoma Ramadhani Issa walipokuwa wakiishi watoto.
Watoto hao walidai kufikishwa kwenye kilinge cha mganga huyo na kufungiwa ndani huku wakilishwa karanga mbichi na ulezi kwa mwezi mzima.
Kama haitoshi walidai mganga alikuwa akiwalimisha na kuwachotesha michanga usiku kucha huku Salim akionesha chale alizochanjwa sehemu za magotini na kichwani.
Mtoto Salim alisema kuwa alimuona mwenzake Laurent akiruka kimiujiza jambolililomshtua na kumfanya atoroke  baada ya kumuona mganga huyo kauacha mlango wazi.
Baadhi ya mazagazaga ndani ya gheto la sangoma huyo.
“Ndani ya nyumba kuna mauzauza mengi sana, wakati mwingine tulikuwa tunasikia sauti za watoto lakini hatukuwaona.
“Hata chakula (karanga na ulezi) tulikuwa tukipewa kingi, lakini tukila kidogo tu kinaisha kama vile tulikuwa tunakula na watu wengine,” alisema Salim.
Mmoja wa watoto waliokuwa kwa sangoma huyo akionyesha makovu ya chale kwa OFM.
Mmoja wa wazazi wa watoto hao ambaye ni Makamu wa Rais wa Chama cha Waganga wa Tiba za Jadi Tanzania (Tameto), Swalehe Issa Bukuku, alisema kuwa watoto hao walifika nyumbani wakiwa katika hali ya kuweweseka huku wakisisitiza walikuwa kwa mganga Igogo na wangeweza kuwapeleka kwa kuwa wanaikumbuka njia waliyopita siku ya kwanza.
Sangoma Rama akiandaa jeans yake baada ya kunaswa na OFM tayari kuelekea kituoni.
OFM na wazazi wa watoto hao pamoja na wanaharakati walifika kwa mganga huyo wakiwa na mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Ujaluoni.
Bahati mbaya mganga huyo alikuwa ametoka hadi ndugu yake alipompigia simu  na kumtaka afike kilingeni baada ya kuambiwa kulikuwa na wateja.
Safari ya kuelekea kituoni.
Mganga huyo alifika kilingeni kwake ndipo OFM ikiwa pamoja na mwenyikiti wa mtaa na wazazi wa watoto hao na Polisi Jamii, walimnasa na kumfikisha Kituo Kikuu cha Polisi cha Nyamagana na kufunguliwa jalada la uchunguzi MW/RB/07/2014 JALADA LA UCHUNGUZI.
Gheto la sangoma Rama kwa nje.
Mganga huyo alidai kwamba hakuwaiba watoto hao bali aliwachukua ili wamsaidie kazi ya kumlisha paka wake huku akikana kuwachanja na kuwafanyisha kazi usiku.
CREDIT: GPL

No comments:

Post a Comment