aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Tuesday, January 28, 2014

MAJANGA:NIMEVURUGWA YA SNURA MUSHI YAPIGWA MARUFUKU KUONESHWA KWENYE TV.

BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA), limeifungia video ya wimbo ‘Nimevurugwa’ya mkali wa muziki wa mduara, Snura Mushi ‘Snura’ kwa madai ya kukosa vigezo vya kimaadili kwa jamii.clip_image002Akizungumza hivi karibuni, Snura alisema hajui ni sababu gani iliyofanya kazi yake kufungiwa kupigwa katika vituo vya televisheni.

“Nilipigiwa simu na rafiki zangu na kuambiwa hivyo, lakini mpaka sasa sijui ni kwa sababu gani maana sioni kama nimefanya kitu cha ajabu katika video hiyo na cha kushangaza hata sijaulizwa na yeyote, ila ndiyo hivyo,” alisema.

Snura alisema wakati amesambaza video ya wimbo wake ‘Majanga’, kuna baadhi ya mashabiki walimshangaa ni kwanini hajacheza katika kazi hiyo kitu kilichosababisha video ya wimbo huo kupooza na kutokuwa na mvuto kwa mashabiki wake.

clip_image001“Nilivyopata malalamiko hayo, nikaona nisiwaboe kwa kuendelea kutoa video ambazo sichezi. Katika wimbo uliofuata nikacheza, kumbe nilikuwa naandaa mazingira ya kufungiwa,” alisema.

Snura ni kati ya wasanii ambao wanafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na televisheni kutokana na ubora wa kazi zake ambazo zinaliteka soko la muziki nchini.
Na hii ndio kazi ya Msanii huyo ambayo Imefungiwa kuchezwa katika Stasheni za Televisheni hapa nchini

No comments:

Post a Comment