aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Sunday, January 5, 2014

MFANYABIASHARA WA KIKE APIGWA RISASI USONI NA KUPORWA MABEGI MAWILI YA HELA KARIAKOO..!!

Damu ya Mfanyabiashara huyo ikiwa imetapakaa katika gari lake baada ya kupigwa risasi na majambazi waliompora kiasi kikubwa cha fedha na kutoweka.
Mfanyabiashara mmoja (Jina Halikufahamika) Mwenye asili ya Asia ameshambuliwa na majabazi (majira ya saa 12 Kasoro jioni )kwa kupigwa risasi katika paji la uso wake na kisha majambazi hao kutoweka na mabegi mawili yaliyoojaa fedha.
Hata hivyo haikujulikana kwa haraka ni kiasi gani cha fedha ambacho kilikuwemo katika mabegi hayo. Wakiongea na mwandishi wetu baadhi ya mashuhuda wa tukio walidai kuwa majambazi hao walikuwa  watatu na mmoja alikuwa na bunduki aina ya SMG

Wakielezea tukio hilo baadhi ya wafanyabiashara wengine katika maeneo hayo ya mtaa wa Lindi na Kongo (Kariakoo) walidai kwamba Mfanyabiashara huyo alitoka na kufunga duka lake huku akiwa na mabegi mawili na Mashine ya kutolea Risiti ya EFD na kuelekea katika gari lake dogo aina ya Suzuki Carry na Ghafla walitokea watu wawili waliokuwa katika pikipiki na mmoja wa tatu alikuwa amesimama pembeni kidogo na gari hiyo na kisha kuelekea moja kwa moja katika gari hiyo na kumpiga risasi mfanya biashara huyo aliyekuwa akijiandaa kuondosha gari lake.


Hata hivyo baadhi ya watu wamelaumu utaratibu wa wafanya biashara wengi wa kariakoo kuhifadhi fedha nyingi katika maduka na badala yake wamewataka wafanya biashara hao kutafuta mbinu mbadala itakayowaezesha kuweka fedha na mali zao salama kabisa ikiwa ni pamoja na kutumia huduma za kuhamisha fedha kwa kutumia mitandao, cheque, na hata credit card kuliko Cash kwani imekuwa kawaida kwa mtukio haya kujirudia eleo hili la Kariakoo.

No comments:

Post a Comment