aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, January 25, 2014

KASHFA YA KUSAGANA KATI YA IRENE UWOYA NA MARIAM ,SOMA ZAIDI


Mariam Ismail
Mastaa wa filamu nchini Mariam Ismail na Irene Uwoya wanadaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi(usagaji) na kudaiwa kuishi pamoja kabisa. wiki kadhaa nyuma muigizaji mmoja chipukizi anayekuja juu kwa kasi aliutonya mtandao huu kwa kusema " Mariam Ismail na Uwoya wanasagana tena wanaishi pamoja kabisa, fuatilieni mtajua".

Baada ya habari hizo ilibidi Swahiliworldplanet kuwatafuta mastaa hao, wa kwanza kutafutwa akiwa Irene Uwoya lakini namba yake ya simu kwa takribani wiki 2 ilikuwa haipatikani na hata jana alipotumiwa ujumbe kupitia namba yake nyingine hakujibu.

Baada ya hapo ilibidi kumtafuta Mariam Ismail ambaye wamecheza filamu nyingi na Irene Uwoya kama vile Sobbing Sound, Omega Confusion, The Return Of Omega na Apple, Hata hivyo Mariam anafanya vizuri katika filamu alionekana kuwa busy na kuchelewa kujibu ujumbe wa madai ya kusagana na Uwoya lakini jana star huyo aliyejipatia umaarufu kwa kuuvaa vizuri uhusika katika filamu zake alitoa ushirikiano mzuri kwa kujibu madai hayo akidai sio kweli ila yeye na Uwoya ni marafiki wa karibu sana na wanasaidiana katika shida na raha ndiyo maana baadhi ya watu wameshaanza kusema vibaya...

"Nadhani mimi ndio mtu wa kwanza kupiga vita upumbavu kama huo... mimi ni mwanamke ambae nimeumbwa kikamilifu.. sina kasoro yoyote ya kunifanya niwe na mwanamke mwenzangu....hao wanaofanya upumbavu huo nadhani wana vijikasoro kwenye mili yao.... Irene Uwoya ni rafiki yangu sana tena urafiki wetu sio wa leo wala kesho... ni marafiki wa kushibana kabisa... nikoseapo huwa ananikosoa na yeye akoseapo huwa namkosoa....sometimes huwa tunagombana na kupatana vitu ambavyo ni vya kawaida katika maisha." alisema Mariam ambaye hajawahi kukumbwa na skendo yoyote ile kabla.  

Irene Uwoya
Mariam ambaye kipaji chake cha filamu hujionyesha waziwazi alimalizia kwa kusema "Irene ananiheshimu sana na mimi humuheshimu sana Irene, imefikia hatua ya mimi na yeye tukakaa chini na kupanga tuishi wote kitu ambacho sioni tatizo na hilo. Ingekua ni chumba kimoja hapo sawa... lakini ni nyumba kubwa yenye kujitosheleza...kila mtu na room yake...tunaishi kwa amani na kwa kushirikiana penye tatizo hulitatua wenyewe bila kumshirikisha mtu.Ukimya wetu na kupatana kwetu kusiwafanye watu kuanza kuhisi upumbavu juu yetu... natumai ujumbe wangu utawafikia mashabiki wangu wote. Asante. In god I trust."

No comments:

Post a Comment