aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Sunday, January 5, 2014

"Nilipata fununu Dk. Mgimwa amekufa kwa kulishwa sumu"...Waziri

Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi, Mkuya alisema ingawa taarifa hizo zimeanza kusambaa, lakini amewataka wananchi kutulia na kuamini kwamba Waziri Mgimwa amekufa kifo cha kawaida.

“Taarifa hizi nimeziona mpaka kwenye vyombo vya habari, lakini nataka kuwaambia kwamba tuamini hii ni safari ya mwanadamu, hata mimi na wewe hapa tunaongea pengine baada ya dakika nne mmoja wetu ataiacha dunia.

“Nawaombeni sana uhai na umautu ni yetu sote wanadamu, tuamini kwamba mwenzetu ametuacha katika hali ya kawaida kabisa,
” alisema Mkuya kwa sauti ya huzuni.

Katika hatua nyingine miezi michache kabla ya kifo chake, Dk. Mgimwa alizungumza na MTANZANIA Jumamosi akiwa Hospitali ya Mediclinic nchini Afrika Kusini kwa matibabu ya kawaida tu.

Akizungumza kupitia simu yake ya kiganjani na kwa sauti isiyo shaka, Dk. Mgimwa aliwataka Watanzania kutokuwa na hofu na afya yake kwani alikwenda hospitali kwa utaratibu wa kawaida wa kuangalia afya yake kila inapobidi.

Taarifa za Dk. Mgimwa kulazwa akiwa mahututi, MTANZANIA ilizipata kutoka vyanzo vya habari ndani ya Wizara ya Fedha na ilipomtafuta mwenyewe akiwa Afrika Kusini alikana kuwa afya yake ni mbaya.


No comments:

Post a Comment