Msanii anaetengeneza mrefu zaidi Tanzaniakupitia muziki wake ‘Diamond Platinumz’ ameelezea sababu zilizompelekea kutoa zawadi ya kuwapeleka shule ya kimataifa watoto walioshinda katika shindano la kucheza ‘Ngololo Style’.
Diamond amefunguka kupitia kipindi chaSun Rise cha 100.5 Times Fm, kinachoendeshwa na Fadhili Haule, Fredwaa, Erick na Samira. Ambapo amedai kuwa wazo hilo lilitoka kwenye mitandao ya kijamii kupitia mashabiki wake walitoa mapendekezo ya zawadi atakayopewa mshindi wa shidano hilo.
“Wakati tunafanya lile tangazo, tulitoa katika mitandao tofauti tofauti, nikawauliza wananchi mnafikiri kitu kipi kizuri ambacho mtoto akishinda apewe, lakini mawazo mengi yalikuwa yanakuja kwamba hao watoto tuangalie katika upande wa kielimu zaidi.” Ameeeleza Diamond.
Amesema alichukua wazo hilo na kulipeleka kwenye menejimenti yake ambayo iliona lina maslahi kwa pande zote na kulipitisha.
“Tukafanya hayo mashindano na kweli watoto hao wakatokea wakashinda, kwa hiyo ikawa ni swala la kutafuta ni shule ipi ambayo itakuwa ni bora na nzuri ambayo watoto watapata elimu bora. Tulichokiangalia sisi ni kwamba aliyekuwepo darasa fulani tutamuendeleza kutoka pale kwenda mbele, na mtu akiwa yuko katika shule ambayo sio International basi sisi tutampeleka International.” Diamond amefunguka.
Akizungumzia suala la kuwaendeleza pia kimuziki watoto hao, Diamond amesema kuwa asingependa watoto hao waishie kidato cha nne kama alivyofikia yeye.
“Unajua tatizo la sanaa, lazima kuna sehemu kwanza inabidi ifikie kwenye level yakielimu ndipo uanze kumuendeleza kimuziki la sivyo utampotosha asisome kabisa. Hata mimi wakati nasoma nilipomaliza darasa la saba mama yangu aliniambia kwamba wewe soma kwanza muziki utafanya.
“Kwa hiyo nikafanya lakini nikawa naconcentrate sana na shule japokuwa nilikuwa naibiaibia kwenye muziki, mpaka nilipomaliza form four ndipo nilipoanza kuingia rasmi katika muziki. Lakini kwa wegine lazima uangalie njia ipi nzuri ambayo itamsaidia mtoto, yule bado mdogo, muziki unanasa na mtu unamvuta kabisa hadi anaacha shule. Hata mimi nisiwe muongo, niliacha shule nikafanya muziki baada ya kumaliza form four.” Hitmaker wa My Number One amefafanua.Diamond atafurahi endapo watoto hao wanaosoma kwa fedha yake watafikia hatua wawe viongozi wakubwa wa nchi na sio lazima wawe wanamuziki.
“Na mimi ntasikia raha hata kesho nikisikia mtoto ambaye kasomeshwa akaja kuwa kesho hata kuwa waziri ambapo ule muziki ndio umemfanya yeye kuwa waziri, na sio lazima awe mwanamuziki.”
Kupitia Instagram, Diamond ameshare picha zinazoonesha akiwakabidhi watoto hao katika shule ya kimataifa ‘East Africa International School’ iliyopo Mikocheni, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment