aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Tuesday, January 21, 2014

ROSE NDAUKA ASHANGAZWA NA TUNDA MAN KUJISIFU KUWA NAE KIMAPENZI.


IMG_9680rrr
MSANII wa filamu nchini Rose Ndauka ashangazwa na kauli ya msanii wa muziki wa bongo Fleva Tunda Man ya kujitangazia kuwa alishawahi kuwa naye  katika mahusiano na kuwa ni mwanamke wa kwanza kuwa naye.Mshangao huo umeibuka mara baada ya TundaMan kueleza kuwa, alishawahi kujihusisha kwenye mahusiano ya kimapenzi na msanii huyo mnamo mwaka 2006.Tundaman alisema hayo kwenye mahojiano yaliyofanyika katika kipindi cha XXL kinachorushwa na Clouds Fm, ambapo aliweka wazi kuwa alishawahi kuwa na mahusiano na mwanadada huyo wakati wote wawili wakiwa bado hawajapata majina kwenye fani zao.Aliendelea kueleza kuwa walikuwa wakikutana na Ndauka katika studio iliyokuwepo maeneo ya Kariakoo ambapo ndipo walipoanza mahusiano yao ya kimapenzi.Akizungumza na jarida hili msanii huyo wa kike Rose Ndauka, ambaye sasa ni mama wa mtoto mmoja wa kike, alisema kuwa amechukizwa na habari hizo kwani hakuzitarajia kwa kipindi hiki ambapo yupo katika ulezi wa mtoto wake.Kutokana na maneno hayo Ndauka aliweka wazi na kusema kuwa Tundaman anatafuta ugomvi kutokana na kauli yake aliyoiongea na kudai kuwa kwa nini asiongee habari hiyo tangu mwanzo kama inaukweli wowote."Alichoongea akina ukweli wowote na ninamshangaa kwa nini atoe kauli hiyo kwa kipindi hichi kama kuna ukweli alikuwa wapi kutotoa ukweli huo hapo mwanzo, ameniudhi sana sitaki maneno maneno na mtu yeyote yule" alisema Ndauka.Aliongezea kuwa anatafuta kuanza kusomwa kwenye magazeti kwa  kuanza kuongea vitu ambavyo havina ukweli kwa lengo la kutaka kuchafuana