Huu ndiyo muonekano wa dampo hilo la kisasa kwa upande wa juu ambapo ujenzi upo katika hatua za mwishoni.
Chemba pekee ambayo ni maalum kwa ajili ya kupitishia takataka zenye kimiminika, pia kupitishia takataka ambazo zitakuwa zimesagwa na kupelekwa katika bwawa maalum litakalotumika kutengenezea umeme pamoja na mabaki mengine ya takataka yatatumika kutengenezea mbolea.
Dampo hilo la kisasa kwa ndani ambapo kwa sasa wameweka kokoto ndogondogo chini huku ujenzi ukiendelea.
Hii ni sehemu ya kupaki magari ambayo yatakuwa yakitupa takataka katika dampo hilo la kisasa.
Pichani ni jinsi takataka kutoka pande mbalimbali za jiji la Mbeya zilivyokuwa zikitupwa kabla ya dampo hilo la kisasa kujengwa katika eneo hilo jirani na mlima Nyoka jijini Mbeya. Dampo hilo la kisasa linategemea kuanza kufanya kazi hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment