aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Tuesday, January 28, 2014

LAANA:MCHUMBA WA MTU ANASWA LIVE AKIFANYA BIASHARA YA NGONO.. ALIAGA ANAENDA KUSALIMIA KWA BIBI..TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA

OPARESHENI Fichua Maovu (OFM)  si mchezo! Safari hii imenasa tukio la mchumba wa mtu aliyetajwa kwa jina moja la Jose kuuza mwili. 
Za mwizi 40: Mchumba wa mtu baada ya kunaswa na OFM akijiuza licha ya kuaga kuwa anakwenda kwa bibi yake.
Tukio hilo lilijiri eneo maarufu la Baa ya Kaumba iliyopo katikati ya mji kwenye Mtaa wa Makongoro, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo OFM na polisi walikuwa kwenye oparesheni za kufichua uovu wa biashara haramu ya ngono.


OFM NOMA: Mchumba wa mtu na wenzake wakiwa mikononi mwa OFM na Polisi.
Kwa mujibu wa mchumba huyo katika mahojiano na OFM, aliaga kwao Kilosa kuwa anakwenda Morogoro mjini kumuuguza bibi yake ambaye ni mgonjwa.
Tofauti na matarajio ya familia yake, mrembo huyo alikwenda kukita kambi maeneo hayo akijihusisha na biashara hiyo haramu eti kwa madai ya kusaka fedha ya kununulia sare za harusi yake ambayo inatarajiwa kufanyika Februari 15, mwaka huu.


Mshangao: Mchumba wa mtu akishangaa baada ya kubambwa na OFM.
Jumatano iliyopita, OFM ilipokea simu kutoka kwa dada mmoja ambaye alieleza kuwa kuna ‘shori’ ambaye ni mchumba wa mtu anajiuza katika viunga vya Kaumba.
Dada huyo aliendelea kueleza kuwa yeye ni mmoja wa wajumbe katika kikao cha harusi ya dada huyo huku akiwa ameshachangia shilingi elfu 50 lakini alishangaa kumuona maeneo hayo hatarishi.


Twendeni: Mchumba wa mtu akiongoza wenzake wanaoshuka kutoka kwenye difenda kuelekea kituoni.
“Niamini mimi, tunakaa naye Mji Mpya (Morogoro). Hata fedha za advance ya ukumbi, vinywaji, MC na muziki tumeshalipa na harusi yake inatarajiwa kufanyika Februari 15, mwaka huu.
Baada ya kunyetishiwa habari hizo, kikosi kazi cha OFM kiliingia mzigoni kwa kushirikiana na dada huyo ambaye alivalishwa ‘beji’ yao na kufanikisha kunaswa kwa mchumba huyo.



Chini ya ulinzi: Mchumba wa mtu na wenzake wakiwa chini ya ulinzi kituoni.
OFM ikishirikiana na polisi wanaojua kujituma kwenye majukumu yao walimtia mbaroni dada huyo akiwa katika pilikapilika zake za kunasa wanaume huku mmoja wa vijana wa OFM akijifanya mteja na kupatana naye bei ya kuingia chumbani kwa ‘shoti taimu’.
Baada ya kunaswa, mwanadada huyo alikiri mbele ya OFM kuwa ni bibi harusi mtarajiwa.
“Jamani… jamani ni kweli mimi ni mchumba wa mtu, shetani ameniponza nisameheni,” alisema.

 Hata hivyo, kilio chake kiligeuka cha samaki kwani hakikusikika, yeye na wenzake walionaswa walipelekwa moja kwa moja katika kituo kikuu cha polisi ili kupisha sheria ichukue mkondo wake

No comments:

Post a Comment