aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Sunday, January 12, 2014

KIGOGO CHADEMA ALIYETEKWA AFICHWA...SOMA ZAIDI HAPA


WENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilaya ya Temeke, Joseph Yona ameondolewa hospitali alikokuwa akipatiwa matibabu na kufichwa kusikojulikana. 

Chanzo cha habari kimelieleza kwamba, Yona ambaye alikuwa amelazwa katika Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI), amehamishwa na familia yake kutokana na sababu za kiusalama.

 

Kwa mujibu wa chanzo hicho, familia imefikia uamuzi wa kumhamisha baada ya kuona watesi wake (wabaya) wanamfuata Yona hospitalini hapo.

Kutokana na mazingira hayo, familia hiyo ililazimika kumuomba daktari aliyekuwa akimhudumia mgonjwa huyo kumruhusu ili waweze kumtibu nyumbani kwao.

“Kutokana na hali hiyo, daktari alimruhusu baada ya kuona hali yake inaendelea kuimarika, licha ya kuwepo kwa majeraha ambayo yasingeweza kumletea matatizo makubwa.

“Familia ya Yona ilimuomba daktari aliyekuwa akimtibia kumruhusu kuondoka, ili aweze kutibiwa na daktari binafsi chini ya uangalizi maalumu wa familia, kwa sababu watesi wake walikuwa wakimfuata hospitalini hapo.”

Chanzo hicho kilichopo karibu na familia hiyo, kilieleza kuwa Yona alitolewa siku ile ile aliyofikishwa hospitali na kufichwa kusikojulikana kwa sababu za kiusalama, baada ya kuwataja watesi wake hadharani.

Hata hivyo, Ofisa Habari wa MOI, Patrick Mvungi alithibitisha kutolewa kwa mgonjwa huyo siku hiyo alipolazwa na kudai kuwa mgonjwa huyo alikuwa akiendelea vizuri.

“Baada ya daktari kumpima na kumuona anaendelea vizuri, wameamua kumruhusu kurudi nyumbani na kwamba mpaka sasa hajarudi tena katika taasisi hiyo,” alisema Mvungi.

Yona alitekwa, kupigwa, kuteswa na watu aliodai ni baadhi ya wanachama wenzake wa chama hicho, kwa madai kuwa amekuwa akishirikiana na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, Zitto Kabwe.

Baada ya kupigwa, Yona alipelekwa katika eneo la Ununio, Tegeta nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na kuokotwa na wasamaria wema wanaoishi karibu na maeneo hayo.

Kutokana na hali hiyo, mgonjwa huyo alipelekwa MOI kwa ajili ya kupatiwa matibabu ambapo alipimwa kwa kipimo cha CT-Scan pamoja na kufanyiwa vipimo vingine vya kitabibu.

Awali akielezea mkasa huo, Yona alisema aliingia katika mgogoro huo baada ya kuitisha kikao cha waandishi wa habari na kuiomba Kamati Kuu ya Chadema kuitisha mkutano wa kujadili suala la Zitto na wenzake.

Mbali ya Zitto, watuhumiwa wengine walikuwa ni aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk. Kitila Mkumbo na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho mkoani ArushaSamson Mwigamba.

Alisema kutokana na hali hiyo, viongozi wakuu wa chama hicho, akiwemo Mwenyekiti, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa walimuita na kumwambia ajitoe ndani ya chama hicho kabla ya kumfukuza,jambo ambalo alilipinga.


Hata hivyo, Dk. Slaa amekanusha madai hayo na kueleza kuwa hajawahi kuwasiliana na Yona kwa lengo la kumshinikiza ajiuzulu wadhifa wake huo.


-MTANZANIA

No comments:

Post a Comment