aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Wednesday, January 22, 2014

LINAH NA SKENDO YA KUTOKA NA KIGOGO

STAA wa Bongo Fleva, Estelinah Sanga ‘Linah’ amepangua skendo inayomtafuna ya kutoka na kigogo mmoja wa wizara nyeti ya Serikali ya Tanzania na kupachikwa ujauzito.

Estelinah Sanga ‘Linah’.

Akizungumza na mwandishi wetu, Januari 17, mwaka huu, Linah alisema shutuma hizo zimemwandama wakati siyo za kweli na hana uhusiano wa kimapenzi na kigogo yeyote wa serikalini.

“Watu wamenizushia mambo kibao kuhusiana na ujauzito wakati sina na wala sijawahi kuwa kwenye uhusiano na kigogo yeyote wa serikalini, hata mtu anayetajwa sijawahi kumuona zaidi ya kumsikia tu.

 
“Naomba nieleweke kuwa nina mchumba wangu na anajulikana hadi kwetu,” alisema Linah.