aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Sunday, January 19, 2014

DOGO YOUNG KILLER AFUNGUKA NA KUSEMA KUWA KWA SASA HAITAJI MPENZI,SOMA ZAIDI UJUE SABABU!


Youngkiller1
Young Killer anasema pamoja na umri wake kumruhusu kuwa mrembo katika maisha yake, bado hafikirii kuanzisha uhusiano na msichana kwa sasa.
“Umri wa kuwa na mpenzi nimeshafikia lakini sasa hivi nafanya mambo yangu halafu baadaye naamini ntakuja kufanya hayo masuala, so sasa hivi najipanga kwanza,” Killer aliiambia Bongo5. “Kusumbuliwa nasumbuliwa sana tu sema kuna msemo mmoja ambao nakuambia wa Fid Q ‘Usiache ulichotaka maishani ghafla tu na kufuata kile ambacho umetamani’. Nimekuja kwaajili ya muziki, nilitegemea utanipa vitu vingi ila sio mademu tu.”
Wakati huo Handsome Boy huyo asiye na matunzo, amesema video ya wimbo wake ‘Mrs Supastaa’ iliyoongozwa na Adam Juma ni moto wa kuotea mbali.
“Ni video kali, naamini katika video zangu zote ile ndio inaweza kuwa video yangu ya kwanza kufanya video kali. Naamini zingine zitakuja ila ile kiukweli kali yaani,” alisema. “Nategemea mashabiki wangu wataipokea vizuri kwasababu ni video nzuri, binafsi nimeridhika nayo, sijawahi kufanya video kama ile.”

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII