aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, December 12, 2013

"Wajinga hunena kwamba CCM ilileta uhuru Tanganyika, Inasikitisha sana"....Profesa Mbele

Kiwango cha ujinga Tanzania kinatisha. Utawasikia wengi wakisema kuwa CCM ilileta Uhuru Tanganyika mwaka 1961.

Wajinga wengine, kuanzia wanasiasa hadi watu wa mitaani, husema kuwa CCM imekuwa madarakani kwa miaka 52.Utamsikia mwanasiasa anaiponda CCM kwa kuuliza, "Miaka yote 52 ya utawala wa CCM, wananchi mmenufaika vipi?" 

 
Na utammsikia kada wa CCM akitamba, "CCM ni chama chenye uzoefu wa miaka 52.

Hapakuwa na CCM mwaka 1961. Chama kilicholeta Uhuru Tanganyika ni TANU. Wala CCM haijawa madarakani miaka 52. Kuna mengi katika historia ya Tanganyika na Tanzania ambayo yanasahaulika au kupotoshwa kwa sababu ya uzembe wa wa-Tanzania.

Wajinga wengine wanasema kuwa tunasherehekea kumbukumbu ya Uhuru wa Tanzania au Tanzania Bara. Mwaka 1961 hapakuwa na nchi iliyoitwa Tanzania wala Tanzania Bara. Nchi iliyopata Uhuru mwaka ule ni Tanganyika. Inasikitisha.