aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, December 14, 2013

KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA UHURU WA TANGANYIKA YALIOANZA 9.12.2013 YAMALIZIKA LEO 14.12.2013 MOSCOW-URUSI.

Chama cha mapinduzi Moscow Urusi leo Desemba 14, 2013 wamekamilisha maadhimisho ya miaka 52 ya uhuru yalioanza December 9, 2013 kwa maonyesho mbalimbali.

   MWENYEKITI WA TAWI LA CCM-MOSCOW
 NDG SALIM MFUNGAHEMA
 Akizungumza na wanachama wa tawi la CCM-Moscow Urusi, Mwenyekiti wa tawi la CCM-Moscow Ndg Salim Amani Mfungahema alisema CCM ni chama bora chenye sera safi na ndicho chama tawala cha serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, alisema kutokana na CCM kuwa chama bora na Ilani yake inatekelezeka vizuri hivyo hatunabudi vijana wa elimu ya juu kukiunga mkono ili kiendelee kushika dola. Ndg Mfungahema alisema kutokana na ubora wa CCM ndio sababu kuu ya mafanikio ya Tanzania kuwa taifa linaloheshimika duniani na kumfanya kila mtanzania duniani ajisikia faraja na utaifa wake. Uimara wa CCM unatokana na misingi bora ya TANU ambayo pasi na mashaka CCM imekua ikiiendeleza kwa vitendo kwa kudumisha misingi ya utawala bora, kudumisha amani, kuweka utawala wa sheria unaojali utu wa mwanadamu na kuwajali raia wake kwa kuondoa kero zao kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuwaletea watanzania maendeleo ya haraka yenye tija.

KATIBU WA TAWI LA CCM-MOSCOW
 NDG HASSAN KAPILIMA
Kwa upande wake katibu wa  tawi Ndg Kapilima alisisitiza umoja na ushirikiano miongoni mwa  wanachama ili kuweka mshikamano katika jamii yetu, umoja na mshikamano ndio siri ya ushindi wa chama chetu alisema katibu. Aliwataka vijana wote kuungana na kumaliza tofauti ndogondogo zilizopo ili tuweze kufikia lengo letu kuu ambalo ni ushindi.

PICHA NA MATUKIO MBALIMBALI 
Mwenyekiti akisisitiza jambo katika moja ya hotuba yake.

Katibu akijibu swali ambalo liliulizwa na mwanachama.

BAADA YA HOTUBA MAMBO YALIENDELEA HIVI UKUMBINI  
KUPATA KINYWAJI NA CHAKULA

Mwenyekiti akiteta jambo na afisa ubalozi ambaye alihudhuria maafari hayo kumwakilisha balozi.

Mwenyekiti Ndg Mfungahema (kulia)akigonga CHEERS na mmoja wa maafisa ubalozi ambao walialikwa.

Katibu wa tawi Ndg Kapilima akibadilishana mawazo na mgeni mwalikwa afisa ubalozi.
Katibu akimkaribisha afisa ubalozi ukumbini.

No comments:

Post a Comment