aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Monday, December 30, 2013

Thomas Ulimwengu noma, amwaga manoti ukumbini


 
 
Mshambuliaji wa TP Mazembe ya DR Congo, Thomas Ulimwengu akigawa manoti.
Na Issa Mnally
MSHAMBULIAJI wa TP Mazembe ya DR Congo alionyesha kweli maisha yake sasa ni ya juu baada ya kumwaga fedha kwa wanamuziki wa bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’.

Ulimwengu alifanya hivyo kwenye shoo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Taifa wa Burudani wa Dar Live, Mbagala-Zakhem, jijini Dar siku ya Boxing Day.
Mshambuliaji huyo wa kutegemewa wa TP Mazembe na Taifa Stars, aliingia ukumbini hapo Saa 4:45 usiku na kuwa kivutio kwa wapenda soka waliokuwa ukumbini.
Makeke ya mchezaji huyo yalianza pale ulipopigwa wimbo wa ‘Mtu Pesa’ kwani aliinuka kutoka katika kiti ambacho alikuwa amekalia na kuteremka ngazi haraka na kukimbilia jukwaani huku akiwa amekamata  pochi mkononi kisha kuwavaa wanamuziki hao na kuwamwagia noti nyekundu tu yaani ‘minoti’.
Ilionyesha kuwa  wimbo huo wa ‘Mtu Pesa’ uliotungwa na Banza Stone ambaye kwa sasa anaitumikia bendi ya Extra Bongo ulimkuna sana mwanasoka huyo wa kimataifa.  

Mbali ya wimbo huo wa Mtu Pesa nyimbo nyingine ambazo zilionekana kumkuna mwanasoka huyo na kushindwa kutulia katika kiti na kucheza ni ‘Jirani’, ‘Mtaa wa kwanza’, ‘Mwana Dar es Salaam’ na ‘Kisa cha Mpemba’.
-GPL 

No comments:

Post a Comment