aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Monday, December 16, 2013

PETER O’TOOLE WA ‘LAWRENCE OF ARABIA’ AFARIKI AKIWA NA MIAKA 81

                                                                   Peter O'Toole enzi za uhai wake.
 MCHEZA sinema Peter O'Toole, aliyeng’aa mnamo mwaka  1962 alipocheza kama T. E. Lawrence katika filamu  ya  "Lawrence of Arabia",  amefariki akiwa na umri wa miaka 81, shirika la BBC limetangaza.O'Toole, alifariki Jumamosi iliyopita (Desemba 14) katika Hospitali ya Wellington, jijini London, baada ya kuugua kwa muda mrefu, jambo ambalo lilithibitishwa na wakala wake, Steve Kenis.
Mwigizaji huyo, mzaliwa wa Ireland, aliyetangaza kuacha sanaa hiyo, aliwahi kushinda tuzo zinazojulikana kama Academy Awards kwa kucheza katika filamu za "Lawrence of Arabia," "Becket" (1964), "The Lion In Winter" (1968), "Goodbye, Mr. Chips" (1969), "The Ruling Class" (1972), "The Stunt Man" (1980), "My Favorite Year" (1982)  na  "Venus" (2006).Pia alishinda tuzo  nne za Golden Globes,  BAFTA  na ya  Emmy,  mbali na kushinda tuzo ya heshima iliyojulikana  kama Honorary Academy Award mwaka  2003.
O'Toole ameacha mabinti  Kate  na Patricia, na mtoto wa kiume Lorcan.

No comments:

Post a Comment