aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Wednesday, December 25, 2013

Picha: wafunga ndoa hadharani wakiwa uchi wa mnyama huko Marekani, waenda kuilia honeymoon lupango



1
Dunia haiishi mambo na vijimambo, bibi na bwana harusi waliojikita katika kutetea haki za kupiga picha uchi, Gypsy Taub na mkewe Jaymz Smith waishio San Francisco wamejikuta wakilia honeymoon yao lupango baada ya kuchojoa nguo zao zote wakati wakifunga ndoa.
Kwa mujibu wa ‘The San Francisco Chronicle, bibi harusi alifika katika eneo la tukio akiwa amevaa nguo kama kawaida lakini alizichojoa zote ghafla na kubaki mtupu kama alivyozaliwa kisha akapaza sauti, “hii ni kwa ajili ya kupinga sheria zanazokataza kuwa mtupu kwa namna ambayo imekuwa katika ndoa.”
Naye mfungishaji ndoa ambaye sio kiongozi wa dini yeyote, alisema “najua watu wa San Francisco wako nyuma yangu,” na kisha kuwaambia wana ndoa hao, “sasa mnaweza ku-kiss na kufanya ngono.”
Gazeti hilo limeripoti kuwa tukio hilo lilifanyika hadharani karibu na makazi ya watu ambapo wanawake wengi na watoto walikuwa wakipita eneo hilo.
Baada ya shangwe za ndoa hiyo, maharusi walichukuliwa na gari la polisi na kupelekwa panapohusika, na ripoti zinasema walifunguliwa mashitaka kwa kosa la  kujiachia watupu hadharani.
Hata hivyo wawili hao waliachiwa baadae huku tarehe za honeymoon zikiwa zimeishia selo.
Lakini waliporudi uraiani waliliambia The San Francisco Chronicle kuwa ndoa yao ilikuwa nzuri na ya kufurahisha.
“It was fantastic…it surpassed all my expectations. It was just an awesome party.” Bwana harusi Taub alijigamba. 

No comments:

Post a Comment