aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, December 21, 2013

KUELEKEA KUFUNGA MWAKA 2013.HII NDIOORODHA YA MASTAA WALIO WAPIGWA MIMBA BILA NDOA


 HII ni funga mwaka! Mastaa wa Kibongo, Jennifer Kyaka ‘Odama’, Recho Haule, Belina Mgeni na Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ wamejikuta wakiumalizia mwaka 2013 wakiwa ‘vitumbo ndii’ licha ya kuwa bado hawajaolewa.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, wasanii hao wamebeba mimba hizo kwa nyakati tofauti na wamekuwa wakijificha kukwepa aibu ya kubeba ujauzito kabla ya kufunga ndoa.                                                                              Belina Mgeni.
 “Wanaona aibu kubeba ujauzito kabla ya ndoa, wamekuwa wakijificha na mbaya zaidi hawataki kujionesha maana wengi wao hawajawatambulisha wachumba wao  kwa wazazi wao,” kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutotaja jina lake.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, mapaparazi wetu waliingia mzigoni kusaka ukweli wa habari hiyo ambapo jitihada zilizaa matunda kwa kupatikana kwa picha za mastaa hao zikionesha tayari vitumbo ndii.
                                                                Jennifer Kyaka ‘Odama’.
Baadhi yao, picha zilionesha mimba zikiwa ni kubwa huku wengine zikionekana ndiyo bado changa. Aunty Lulu, Belina walionekana dhahiri kuwa ni waleo au kesho, matumbo yao yalionekana ‘live’ ni makubwa, Odama yeye ilionekana bado halijajitokeza vizuri.
                                                                             Recho Haule. Kwa upande wa Recho Haule, rafiki wa karibu aliyeomba hifadhi ya jina, alipenyeza habari kuwa mimba aliyonayo shosti wake huyo ni ya mpenzi wake wa kitambo, Saguda George lakini naye amekuwa akijifungia ndani kukwepa macho ya watu.
“Recho ni mjamzito lakini amekuwa akijificha kukwepa kamera za mapaparazi si unajua tena uchumba wake na Sagunda kila mmoja alikuwa akiufatilia magazetini!”
                               Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’. Baada ya mapaparazi wetu kujitosheleza na ushahidi wa picha, zoezi la kuwasaka wasanii hao ili kujua wahusika wa mimba hizo lakini simu zao ziliita muda mrefu bila kupokelewa.
Baadhi ya mashabiki walioongea , hawakusita kuonesha hisia zao kwa mastaa hao, kila mtu alikuwa na mtazamo wake juu ya mastaa hao.
 “Unajua kama Belina naona amebeba mimba ila yuko kwenye process ya kufunga ndoa ingawa sijui ni lini kwani niliwahi kumsikia akisema kuwa anaweza kufunga ndoa soon” alisema shabiki mmoja, mwingine akasema hivi:
“Sisi tujuavyo kioo cha jamii maana yake ni mtu kufanya yale yanayofaa kuigwa lakini kwa hawa mastaa wetu  wamefanya tofauti, wote wamebeba mimba bila ndoa, sasa jamii itajifunza nini kutoka kwao?”


No comments:

Post a Comment