aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, December 20, 2013

SIRI YA FIGA BOMBA YA LULU YAFICHUKA!


 SIRI ya muonekano mzuri wa msanii wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ imefichuka baada ya kubainika kuwa, amekuwa akifanya mazoezi kila siku kwa kwenda gym. 
Lulu akifanya mazoezi.
Lulu alianika siri hiyo hivi karibuni kupitia mtandao wa instargram kwa kutupia picha zikimuonesha akiwa kwenye tizi na baadae alipozi na kujifotoa picha ambazo zilimuonesha akiwa na umbo la kuvutia zaidi huku zikisindikizwa na maneno yasemayo; ‘ndiyo siri ya urembo’.
Hata hivyo, baadhi ya watu walioziona picha hizo walimpongeza kwa uamuzi wake huo huku ushauri pia ukitolewa kwa kila mmoja kujali afya yake kwa kufanya mazoezi pale muda unapopatikana.