aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, December 21, 2013

MKE AMFUMANIA MUMEWE AKINGONOKA NA KIMADA GESTI



Mfanyabiashara wa madini aliyefahamika kwa jina moja la Jimmy amejikuta katika wakati mgumu baada ya kufumaniwa na mkewe akiwa na kimada gesti.

 Tukio hilo lililofunga mtaa kwa kujaza wambea kibao, lilitokea hivi karibuni ndani ya gesti moja  Kinondoni jijini Dar es salaam ambapo mke wa mfanyabiashara huyo (jina halikupatikana mara moja), alimnasa mumewe  akijiandaa kuvunja amri ya sita ya Muumba.

Wadakuzi waliokuwa eneo la balaa walitonya kuwa, siku hiyo ya tukio, Jimmy ambaye ni mkazi wa jijini Arusha, alifika Dar kibiashara na baadaye alimsaka kimada huyo wa siku nyingi na kwenda kujirusha naye bila kujua mkewe alishatonywa juu ya usaliti wake.
 
Jimmy kabla ya kuingia gesti inadaiwa alijipumzisha katika grosari iliyo karibu na Mango Garden Bar, baadaye akaenda kwenye gesti hiyo ya jirani bila kujua mkewe alikuwa akitua mguu kila pale yeye aliponyanyua, akazama ndani ya gesti hiyo na kuanza kujiandaa kwa zinaa.
  
 Mke wa Jimmy hakuwa mbali, baada ya kujiridhisha mumewe amezama chumbani, dakika kadhaa na yeye alitokea na kugonga mlango wa chumba hicho kufuatia kutonywa na mhudumu mmoja wa gesti hiyo.
 
Jimmy alikutwa tayari ameshavua nguo zote na kubakiwa na ‘boksa’ huku kimada naye akiwa na ‘kufuli’ pekee.
 
Kilichofuata hapo ni kipigo, mke wa Jimmy alianza kumtembezea kipigo yule kimada. Waandishi nao walivamia na kutandika picha za timbwili ambapo Jimmy alifanikiwa kupenya mlangoni na kukimbia bila kujali nguo nyingine.
 
Kutokana na kelele za timbwili hilo, majirani wa eneo hilo walifika kuhoji kulikoni ambapo mfumaniaji huyo alitoboa siri kwamba amekuwa akimfuatilia mumewe kwa siku nyingi baada ya kuambiwa ana kimada Dar.
 
Wakati pakichimbika, kimada huyo alisikika akimlaumu Jimmy kwamba amemuingiza kwenye mkenge akijua mkewe ni mdodosaji wa mambo na anaweza kufika Dar madai ambayo hayakuwa na wa kuyajibu.

No comments:

Post a Comment