aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, December 12, 2013

Kijana Anusurika Kuuawa baada ya kunaswa Akimbaka Denti wa miaka 14 Usiku na Mchana huko Jijini Arusha..!!

MWANAUME anayedaiwa kuwa ni kinara wa ubakaji jijini hapa, Said (30) mkazi wa Mbauda, amenusurika kifo kwa kipigo kutoka kwa raia wenye hasira baada ya kunaswa akitoka kumbaka denti wa kidato cha pili hadi kupoteza fahamu.


Said anayetajwa kuwa ‘mwenyekiti’ wa kundi linalojihusisha na ubakaji, alishambuliwa na wananchi hao baada ya yeye na wenzake watano kukutwa kwenye nyumba inayodaiwa kuwa ya uhalifu iliyopo Muriet, Bon City jijini hapa wakimfanyia kitendo hicho cha kinyama mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 14.

Mashuhuda wa tukio hilo, akiwemo Mwenyekiti wa Mtaa, Francis Mbise walieleza kuwa mtuhumiwa huyo akiwa na wenzake hao walimbaka usiku kucha msichana huyo aliyetajwa kwa jina moja la Jack, mkazi wa Kwamorombo baada ya kufanikiwa kumrubuni kwa maneno na kumwingiza kwenye nyumba hiyo.

Baada ya kufanya unyama huo usiku kucha, alfajiri  mtuhumiwa huyo alionekana akitoka ndani ya nyumba hiyo akiwa kifua wazi na kukimbia, ndipo wananchi walipomtilia shaka na kumkimbiza na baada ya kukamatwa, aliulizwa kama ni mwizi akakataa  bali alitoka kufanya mapenzi na msichana.

Mbise alisema kuwa wananchi hao waliongozana naye hadi kwenye nyumba hiyo na kumkuta msichana huyo akiwa amelala hajitambui huku sehemu zake za siri zikitoka damu.
Mwenyekiti huyo alisema walipomuhoji kwa nini alikuwa akikimbia, alisema yeye alihofu kuwa msichana waliyembaka amepoteza maisha baada ya kushtuka usingizini na kumwona hajitambui huku wenzake wakiwa hawapo.

Alisema mtuhumiwa huyo alikiri kuunda kundi la ubakaji lenye watu watano likiongozwa na yeye huku wakigeuza makazi ya mmoja wa wahalifu hao kuwa danguro la ubakaji. Ndipo wananchi hao walipoamua kumshushia kipigo cha nguvu kabla ya polisi kufika na kumuokoa.

Watuhumiwa wengine walifanikiwa kukimbia na kutotambulika, lakini wananchi wa eneo hilo wanaendelea
kuwasaka.


Mtuhumiwa huyo alichukuliwa na polisi wenye silaha ndani ya gari aina ya Land Rover lenye namba ya usajili PT 1177 huku akiwa ametapakaa damu usoni.

CREDIT: GPL