aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, December 13, 2013

MZEE SMALL: WALIONIUA NIKIWA HAI, WAMENIONYESHA MAPENZI

Kutoka kushoto ni Mhariri wa Championi Jumatano, Phillip Nkini, Mzee Small, Mhariri Kiongozi wa Magazeti ya Championi, Saleh Ally na Mwandidhi wa Championi, Hans Mloli wakiwa wanaelekea nyumbani kwa Small.

KUZAGAA kwa taarifa za kufariki dunia kwa Mzee Small kuliwachanganya watu wengi sana, lakini bado ilionekana hakuna uhakika katika suala hilo.
                                                  Mzee Small na Saleh wakijuzana baadhi ya mambo.
Taarifa za kifo chake zilianza kuzagaa Jumanne, saa 4 usiku na ilielezwa amefariki muda mchache uliopita na msiba ulikuwa nyumbani kwake Tabata jijini Dar es Salaam.
Kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele, taarifa za kifo cha Mzee Small ziliendelea kuenea kwa kasi kubwa huku kwenye mitandao ya kijamii zikipata nafasi kubwa.
Achana na blogu mbalimbali kuanza kuandika kuhusiana na ‘kifo’ hicho, kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook, Instagram na Twitter, watu mbalimbali wakiwemo wasanii maarufu walikuwa wakiweka picha zake na kumuombea apumzike kwa amani (R.I.P).
                                           Mzee Small akiionyesha timu 
ya Championi jinsi bega lake lilivyopooza.
Gazeti hili mara moja lilianza kufuatilia kutaka kujua kuhusiana na ukweli, mafanikio ya kwanza yalikuwa ni kuzungumza na mwanaye aitwaye Yunus, ingawa alikuwa amelala, aliamka na kupokea simu ya Championi na kusema mzee wake ni mzima.

Lakini gazeti hili harikudhika, juhudi zikafanyika hadi kumpata mkewe, Mama Said ambaye alithibitisha kwamba mumewe, Said Ngamba au Mzee Small ni mzima na alikuwa amelala.
                                         Small (katikati) akisalimiana na Nkini (kushoto) na Saleh (kulia).
“Lakini unaweza usiamini, ngoja basi nimuamshe ili upate uhakika,” alisema na kusikika akimuita, “Mzee Small, Mzee Small, zungumza na huyu ndugu yako.”

“Mzee Small hapa, mimi ni mzima. Taarifa ulizosikia si sahihi,” alisema Mzee Small mara baada ya kuichukua simu.
                           Mke wa Mzee Small, Mama Said akiwa ameketi barazani nyumbani kwake Tabata.
Baadaye akasikika tena Mama Said akisema: “Nafikiri umemsikia baba, basi tumuache apumzike.”

Ushirikiano huo wa Mama Said ulitoa hofu ya taarifa hizo za kifo zilizokuwa zikienezwa huku haijulikani yupi aliyekuwa ameamua kufanya hivyo na kusambaza taarifa zisizokuwa na uhakika.

Juzi mchana, timu ya Championi ilifika nyumbani kwa Mzee Small eneo la Tabata kumtembelea, kubadilishana naye mawazo, kumpa pole na kutoa mchango kidogo kumsaidia matibabu (si lazima kusema kiasi gani).

Baada ya kufika Tabata, timu ya gazeti hili ikiongozwa na Mhariri Kiongozi, Mhariri wa Championi Jumatano, Phillip Nkini na waandishi wawili, Khatimu Naheka na Hans Mloli, ilipewa taarifa Mzee Small alikuwa amekwenda mazoezini.

Mipango ya kumfuata ilianza, lakini ghafla Mzee Small aliwasili akiwa katika pikipiki na kupokelewa na baadhi ya majirani zake ambao amekuwa akiwatania ni wachumba zake.

Mzee Small alisaidiwa kushuka kwenye pikipiki na baada ya hapo akaambiwa kuna wageni wake kutoka Championi. Aliwapokea na mazungumzo yakaanza kabla ya yeye kuomba akapunguze nywele zake.

“Mke wangu amekuwa akiniambia kwamba hizi nywele si nzuri, zimekaa vibaya. Si unaona, nafikiri tungekwenda nikapunguze kidogo halafu wote tutakwenda nyumbani,” alisema na wote wakakubali.

                                               Mzee Small akirejeshwa na pikipiki (bodaboda) akitokea mazoezini.
Kwa kinyozi hapakuwa mbali, Mzee Small aliingia pamoja na timu nzima ya Championi, wakati wakinyoa mazungumzo yalianza na akaanza kusimulia mkasa huo wa kuzushiwa kifo akiuita ni bomu.

“Hili bomu la leo la kuzushiwa kifo limeniweka katika wakati mgumu, watu wamekuwa wakipiga simu mfululizo wanataka kujua kama ni hai au la.

“Nimeshangazwa sana, nilitaka kujua huyo aliyezusha hayo yote ni nani, lakini naweza kusema nawashukuru hao waliozusha maana wamenionyesha kitu kimoja ambacho sikutegemea.

“Mapenzi ya watu kwangu, kweli watu wengi wamenipigia sana wakitaka kujua kama ni kweli au la, naendeleaje na kwa nini imekuwa hivyo. Hadi sasa simu zinaendelea kuingia, kumbe kuna Watanzania wanaonijali.

“Hakika maisha ni magumu, nateseka lakini angalau nina nafuu na kila siku, mara mbili, asubuhi na jioni natakiwa kufanya mazoezi,” anasema Mzee Small.

source:gpl

No comments:

Post a Comment