aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Sunday, December 8, 2013

Meli ndogo ya mizigo yazama kilwa masoko....mtu mmoja hajulikani haliko



Mtu mmoja aliefahamika kwa Jina la Nice Mtega fundi mkuu wa Meli ndogo ya mizigo iitwayo MV MERCI II inayomilikiwa na Semuhungu Shingiro anahofiwa kufa maji baada ya kutoweka toka kuzama kwa meli hiyo katika bandari ya Kilwa masoko.
 
 Akiongea na mwandishi wetu, meneja wa Bandari ya Kilwa, Bw. Iddi Omary,  alieleza kuwa Meli hiyo iliyofunga gati jana jioni ikitokea songosongo na  kupakia tani 30 za mchanga na tani 30 za maji ilizama majira ya saa 6 usiku wa kuamkia leo ambapo Nahodha wa Meli hiyo Captain Charles Kalinga na wasaidizi wake 3 walifanikiwa kutoka ila Nice Mtega aliekuwepo ndani hajaonekana hadi sasa. 

Juhudi za kumtafuta na kuinua meli hiyo zinaendelea. Sababu ya kuzama kwake bado hazijajulikana
 
 
 

No comments:

Post a Comment