aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, December 5, 2013

WASANII WAMTAKA RAY AACHIE UONGOZI KWENYE UCHAGUZI UTAKAOFANYIKA LEO KUTOKANA NA SKENDO ZAKE CHAFU....

Msanii wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ anadaiwa kulipasua Kundi la Bongo Movie kutokana na uchaguzi wa kundi hilo unaotarajiwa kufanyika leo katika Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar. 
Vincent Kigosi ‘Ray’.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, baadhi ya wasanii wa filamu wanaounda kundi hilo wanadai Ray hafai kuliongoza kutokana na skendo ya kuwagonganisha mademu inayomtafuna huku wengine wakimuunga mkono.
Kuna baadhi yetu wamekuwa wakikaa vikao ili kutaka kumweka pembeni Ray kwa kuwa ameshindwa kuleta umoja ndani ya Bongo Movie na amekuwa akifanya mambo yasiyokubalika…” alisema mmoja wa wasanii ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini.
Chanzo hicho kimesema kwamba wasanii wasiomtaka Ray wamekuwa wakiweka vikao usiku katika kumbi mbalimbali za burudani za jijini Dar kwa ajili ya kumng’oa kwenye cheo hicho.
Wasanii wanaomkubali  Ray wanadai anastahili  kuendelea kuliongoza kundi hilo kwa kuwa ana msimamo thabiti na hakuna mwingine anayeweza kuliongoza.
Msanii wa filamu za Kibongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere, amesema uongozi wa Ray unafika kikomo na wanatakiwa kumchagua kiongozi mpya au  kuendelea naye na jukumu hilo liko mikononi mwa wasanii wenyewe.
“Kimtazamo Bongo Movie linaenda vibaya na hii siyo kwa sababu ya Ray, bali wasanii wote  ni jukumu letu kulijengea heshima kundi hilo, katika uchaguzi wa leo Ray anaweza kuchaguliwa au asichaguliwe kwani kura ni demokrasia…” alisema Steve Nyerere.
Ray hakuweza kupatikana mara moja kuuzungumzia mpasuko huo ndani ya Kundi la Bongo Muvi. 


 GPL

No comments:

Post a Comment