aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, December 12, 2013

Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Jijini Mbeya Mbozi Ajiunga CHADEMA

ALIYEKUWA Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Gabriel Kimollo amejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Kimollo, alisema amechoshwa na ubabaishaji wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutokana na kushindwa kusimamia haki za wakulima wa kahawa.


Alisema anaamini kujiunga kwake na CHADEMA itakuwa fursa nzuri kwake katika kupigania haki za wanyonge ambazo CCM kwa kipindi cha miaka 52 imeshindwa kufanya hivyo.

Alisema ameamua kujiunga na chama hicho, akiamini kuwa ndicho kinaweza kusimamia demokrasia ya kweli, kitamsaidia katika vita yake ya kumkomboa mkulima wa kahawa ambaye anadhulimiwa haki yake katika uuzaji wa zao hilo.

“Nimejiondoa CCM kutokana na mtizamo wangu wa kupinga biashara ya uuzaji wa kahawa usiofuata utaratibu, na ambao naamini usingeweza kumsaidia mwananchi hususani kumkomboa katika dimbwi la umasikini wilayani  Mbozi,” alisema Kimollo.

Alisema aliwahi kutumikia nafasi ya ukuu wa wilaya katika wilaya za Namtumbo, Makete na Mbozi kuanzia mwaka 1999 hadi 2012, ambapo alikoma kufanya kazi hiyo kutokana na kutoelewana na baadhi ya viongozi wa CCM.

Kwa mujibu wa Kimollo, anaamini kuwa bado ana nguvu na uwezo, hivyo yuko tayari kuwatumikia wananchi ambao wanahitaji ukombozi.

Akimkabidhi Kimollo kadi ya CHADEMA, Mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu, alimpongeza akisema kitendo alichokifanya ni cha kijasiri

No comments:

Post a Comment