aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, December 13, 2013

IVO MAPUNDA NA DONALD MUSOTI WAJIUNGA RASMI NA SIMBA SC

KIPA Ivo Philip Mapunda, amesaini Mkataba wa kujiunga na klabu ya Simba SC ya Dar es Salaam,akitokea Gor Mahia ya Kenya.Ivo amesaini Simba SC, baada ya kung’ara akiwa na kikosi cha Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge mwaka huu.
Ivo aliiongoza Kilimanjaro Stars kufika Nusu Fainali ya Challenge baada ya kuwatoa waliokuwa mabingwa watetezi Uganda ‘The Cranes’ kwa penalti 3-2 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90, kipa huyo akicheza mikwaju miwili.
Ivo alisema kwamba ameamua kusaini timu hiyo yenye makao makuu mtaa wa Msimbazi baada ya kuridhishwa na maslahi aliyopewa.Ivo alisema kwamba Simba SC ni timu kubwa na anaamini atafanya vizuri. Ivo pia amewahi kuidakia Yanga SC.

No comments:

Post a Comment