aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Monday, December 9, 2013

Hatimaye Bunge lasitisha shughuli zake na kutoa azimio la kumuenzi Rais Nelson Mandela.....!!

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juzi lilisitisha shughuli zake na kutoa Azimio kutokana na kifo cha Mandela, kwa kumuenzi kwa kudumisha umoja, amani, mshikamano ili kuleta maendeleo.
 
Wakichangia Azimio hilo, wabunge wametaka kutokana na kifo cha mpigania uhuru huyo kujifunza kwa kutolipiza kisasi kwa kusameheana na kuvumiliana katika kila jambo, hususan suala la Katiba na mijadala mbalimbali.
 
Awali, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Edward Lowassa aliwasilisha azimio hilo la kuungana na nchi ya Afrika Kusini, kuomboleza kifo cha muasisi, mpinga ubaguzi wa rangi na Rais wa Kwanza mweusi wa Afrika Kusini.
  
Alisema, “Mandela aliyatoa maisha yake kupigania uhuru wa Waafrika na kupinga ubaguzi wa rangi uliokuwa ukiendeshwa na utawala wa wazungu wachache nchini Afrika Kusini, hali iliyofanya kufungwa katika Gereza la Robben tangu mwaka 1964”.
 
Mandela alizaliwa mwaka 1918 na kufungwa kwa miaka 27. Baada ya kutangazwa kuwa Rais wa nchi hiyo mwaka 1990, alionesha ukomavu wa uongozi kwa kusamehe wote waliomtesa gerezani na kuwaunganisha watu wa nchi hiyo weusi na weupe.
 
Mwaka 1999 alistaafu mwenyewe urais na kurithisha madaraka kidemokrasia hivyo kwa azimio hilo Bunge litamuenzi kwa utu na kuthamini wengine.
 
Alisema Bunge linaazimia kuungana na familia yake, wananchi wa Afrika Kusini na dunia nzima katika kuomboleza msiba wa Nelson Mandela, kwani amekufa, lakini ataendelea kuishi katika mioyo yetu kwa miaka mingi.
 
Wakichangia na kuunga mkono azimio hilo lililopitishwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda ambaye alitangaza kulipeleka katika Bunge la nchini Afrika Kusini, wabunge waliungana katika kuomboleza na kusema bara limepoteza mtu muhimu.
 
Mbunge wa Jimbo la Mkanyageni, Habibu Mnyaa (CUF) alisema kifo cha Mandela kimeunganisha watu wa mataifa yote duniani, hasa waliochukia unyanyasaji, bila kujali wapo umbali gani.
 

“Hata baada ya kifo pia ameunganisha dunia kwa nchi zote hata zenye mitazamo tofauti kupeperusha bendera nusu mlingoti na kuungana kuomboleza,” alisema Mnyaa. 
-Habari leo.

No comments:

Post a Comment