aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, December 5, 2013

ABDU KIBA MBARONI KWA SIMU YA WIZI

KIJANA aliyefahamika kwa jina la Abdul Kiba amejikuta katika wakati mgumu baada ya kukamatwa akiwa na simu inayodaiwa kuwa ni ya wizi na ‘kuswekwa’ sero kufuatia jitihada za ndugu zake kumuwekea mdhamana kugonga mwamba, Ijumaa limetonywa. 
Abdul Kiba.
Tukio hilo lilijiri Jumanne ya wiki hii katika viwanja vya Karume jijini Dar, wakati kijana huyo alipokuwa akicheza mpira. 
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini kilichokuwa uwanjani hapo, muda mfupi baada ya mchezo huo kumalizika, ndipo Abdu akawekwa chini ya ulinzi wa polisi wa kituo cha Msimbazi,  kwa tuhuma ya kuwa na simu ya wizi aina ya Samsung Galaxy yenye thamani ya  shilingi laki nane,  ambayo inadaiwa kuwa mali ya mfanyabiashara aliyetajwa kwa jina la Abdallah Muhidini.
Katika mahojiano yake na Polisi, Abdul alijitetea kuwa simu hiyo aliuziwa na vijana wawili siku za hivi karibuni aliowataja kwa majina ya Shaaban Rajab au Kibabu kama anavyojulikana kwa wengi (anayeshikiliwa na polisi).
Hata hivyo licha ya utetezi huo, Abdul alifunguliwa kesi jalada Na. MS/RB/12267/2013 WIZI KUTOKA MAUNGONI.
Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, ACP Juma Bwire alithibitisha kukamatwa Abdul Kiba na kwamba upelelezi bado unaendelea.
-GPL 

No comments:

Post a Comment