aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, January 10, 2014

"Chadema vumilianeni "....Makamba

WAKATI mgogoro ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ukishika kasi ya ajabu, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yussuf Makamba, amejitokeza na kuwataka viongozi wa chama hicho kuvumiliana na kuacha siasa za kibabe.

Akizungumza kwa hisia katika mahojiano na RAI yaliyofanyika nyumbani kwake Tegeta Wazo jijini Dar es Salaam, Makamba aliuzungumzia mgogoro huo kuwa hauna tija kwa taifa, badala yake unachochea uhasama miongoni mwa viongozi na wanachama wa Chadema.

 
Makamba alisema ameshangazwa kusikia watu wanaomuunga mkono aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe, wanapigwa, wanatekwa na kutupwa porini.

Alisema kinachofanyika ndani ya Chadema hivi sasa si sawa na kinatoa picha mbaya mbele ya safari.

“Kwenye siasa ni kuvumiliana, mnaendesha siasa kwa uvumilivu, kama hivi watu wa Zitto wanapigwa, wanatekwa, wanatupwa porini... mnatafuta nini? Msiendeshe siasa kibabe.

Hivi bado mnapigana mapema... hii si nzuri, tuendeshe siasa kwa utaratibu jamani,” alisema Makamba.

Vurugu zinazoendelea sasa ndani ya Chadema kati ya uongozi na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Zitto, zimesababisha wafuasi wa chama hicho kugawanyika pande mbili baadhi wakiunga mkono uamuzi wa kumvua madaraka au kumfukuza Zitto wengine wakipinga.

Vurugu hizo zimeshika kasi zaidi baada ya Zitto kupeleka maombi yake mahakamani kuizuia Kamati Kuu (CC) ya Chadema kumjadili au kuchukua uamuzi wowote kuhusu uanachama wake.

Kufuatia zuio hilo ambalo limekubaliwa na Mahakama Kuu, vurugu kubwa na mapambano zimezuka kati ya wafuasi wanaoumuunga mkono Zitto na wale wanaounga mkono uongozi wa juu, zilizoanza mahakamani na kusababisha watu wawili kujeruhiwa.

Mgogoro huo pia umehusishwa kutekwa, kuteswa na kujeruhiwa kwa Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Temeke na Mjumbe wa Baraza Kuu, Joseph Yona.

Hatua za awali za upelelezi juu ya tukio hilo kwa mujibu wa polisi, kimazingira zinaonesha kuwa linatoikana na mgogoro unaoendelea ndani ya Chadema, huku kukiwa hakuna chanzo kingine kinachohusishwa.

No comments:

Post a Comment