aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, January 10, 2014

SAMAHANI PICHA ZINATISHA!!!! HAWA NDIO MAJAMBAZI WATATU WALIOUAWA NA KUCHOMWA HUKO MOROGORO....

 
 
 










WANANCHI wenye hasira wa Kijiji cha Kisiwa Kata ya Kiloka Wilaya ya Morogoro Vijini jana usiku wamewauwa kisha kuwachoma moto watu watu  wanaosadikiwa kuwa majambazi.
 
Akizungumza na Mtandao huu shuhuda wa tukio hilo Bw Shabani Mango alisema majambazi hao walivunja nyumba ya mkazi mmoja wa kijijini hicho na kuiba shilingi  490,000.
 
"Jamaa walifka hapa majira ya saa 8 usiku wakiwa na pikipiki Feko yenye namba za usajiri T310 BTC wakipakizana mshikaki,walivunga geni na kuingia ndani ambapo walipora kiasi hicho cha fedha "alisema Mango na kuongeza" Fedha hizo Mwalimu Said Swale Tajiri alizikopa jana mchana kwenye saccos ya Moboto kwa lengo la kumlipia ada mdogo wake anayesoma jijini Dar es salaam leo ijumaa alipanga kwenda Dar kulipa ada nahisi jamaa walipata taarifa kwamba Ticha ana mzigo ndani"alisema Bw Mango.
 
Akihojiwa na mtndao huu afisa mmoja wa jeshi la polisi alithibitissha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja majambazi hao kuwa ni Emmanuel Mlapoli na Kessy Benno ambaye ni boda boda naye pack Pangawe jeshini.
 
''Jambazi mmoja jina lake bado halijafahamika na kwamba eneo la tukio tulikuta pikipiki aina ya Feko yenye namba za usajiri T 3710 BTC mali ya marehemu Kessy Benno ambaye ni makzi wa Kingulwila stesheni manispaa ya Morogoro'alisema Afande huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake kwakuwa sio msemaji wa jeshi hilo. 
CREDIT: MATUKIO NA MICHAPO BLOG

No comments:

Post a Comment