aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Wednesday, January 1, 2014

MUME ADAIWA KUUZA KABURI LA MAREHEMU MKE WAKEKaburi la Aisha Abdul aliyefariki Julai 21, 2004.
Shakoor Jongo na Deogratius Mongela
Hii ndiyo kali ya kufungia mwaka katika zote zilizotokea mwaka 2013! Mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Abrahaman, mkazi wa Kimara-Kilungule, Dar, anadaiwa kuuza kiwanja ambacho ndani yake kuna kaburi marehemu mkewe, Aisha Abdul aliyefariki Julai 21, 2004.
Watoto wa marehemu wakiwa katika kaburi la mama yao.
MALALAMIKO MEZANI
Wakizungumza na Uwazi kwa nyakati tofauti, watoto wa marehemu ambao wanapingana na tukio hilo la baba yao kuuza eneo hilo ambalo ni mali ya marehemu mama yao, walidai kuwa wamefedheshwa na kitendo hicho.

“Kiukweli alichokifanya baba siyo sawa. Haiwezekani auze eneo ambalo lipo kaburi la mama yetu. Mbaya zaidi hadi sisi watoto wa kutuzaa yeye mwenyewe anatutishia maisha.
“Anatufukuza katika nyumba kisa kwa nini tunamuhoji tabia yake ya kuuza maeneo aliyoyaacha marehemu mama,” alisema Tunu ambaye ndiyo msimamizi mkuu wa mirathi.
Kaburi linalodaiwa kuuzwa.
Watoto hao walidai kuwa baba yao anauza mali huku akijua kabisa mama yao aliacha wosia juu ya nani mrithi wa mali hizo (kopi ya wosia tunayo).
“Hatujui nini kimemkumba baba maana amekuwa mkatili asiyekuwa na huruma ya aina yoyote kwetu hadi na kwa majirani,” walisema watoto hao.

USHUHUDA
Gazeti hili lilifika eneo la tukio na kulishuhudia kaburi hilo huku watoto hao wakipiga nalo picha kwa woga wasikute na aliyeuziwa.
Pia majirani walithibisha ukali wa baba huyo katika siku za hivi karibuni.

Katika hali ya kushangaza, wakati watoto hao wakitoa malalamiko hayo walianza kugawanyika kifamilia ambapo mmoja wa mwisho wa kiume alikuwa upande wa baba akiunga mkoni kile alichokifanya mzazi wake huyo.
Baada ya kusikia malalamiko hayo na kuoneshwa vielelezo, ilibidi kumtafuta mume huyo wa marehemu ili kuthibitisha madai hayo.

Alipopatikana alipelekewa tuhuma zake juu ya sakata ambapo bila hata kusikia kwa makini alichokuwa akielezwa alianza kutukana huku akilichimba mkwara Uwazi kufuatilia habari zake.
“Endeleeni kunifuatilia lakini mtakachokiona nisilaumiwe,” alisema baba huyo aliyeonekana kuwa na umri mkubwa.

Katika hitimisho, watoto hao walishauriwa kwenda kwenye vyombo au mamlaka za kisheria ili kupata haki zao.